Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Emmanuel Mkongo amewaagiza wakuu wa idara ya Elimu Sekondari na Msingi kuzipa kipaombele shule za pembezoni zenye mazingira magumu katika mgao wa fedha za lipa kwa matokeo (P4R) zinazotoka Serikali kuu .
Mkurugenzi Mkongo ametoa agizo hilo alipotembelea shule ya Msingi Kisimiri juu ambayo ni miongoni mwa shule za pembezoni katika Halmashauri ya Meru na kubaini changamoto za madarasa, nyumba za Walimu ,vyoo na barabara .
Aidha Mkongo ameahidi kuzifanyia kazi changamoto hizo kulingana na bajeti ya Halmashauri kwani shule nyingi zinachangamoto ya miondombinu.
Mkongo Ameongeza kuwa Serikali imelipa kipaombele swala la Elimu kwa kutoa elimu bila malipo ambapo wanafunzi wengi haswa wanaotoka katika familia za wanyonge wamenufaika.
Naye Ofisa Elimu Msingi kwenye Halmashauri hiyo, Mwl.Sara Kibwana amepokea agizo la Mkurugenzi na kutoa rai kwa jamii na wadau wa Elimu kuanzisha ujenzi wa miundombinu ya Elimu mashuleni jambo litakalo harakisha ukamilishaji "Serikali imekua ikitoa fedha za P4R kwaajili ya kukamilisha miradi iliyoanzishwa na jamii " ameongeza Mwl.Kibwana.
Nao Walimu wa Shule ya Msingi Kisimiri juu wamempongeza Mkurugenzi Mkongo kutembelea Shule hiyo wakidai ni ugeni mkubwa ambao hawakuwahi kuupata kwa muda mrefu hivyi wanapata hamasa ya kutekeleza majukumu yao.
Shule ya Kusimiri juu inajumla ya Wanafunzi 544 na Walimu 11
Ikumbukwe kuwa Serikali ya awamu ya tano imekua ikiwaelekeza watendaji wake kutokukaa maofisini balu kuiendea jamii na kutatua changamoto zinazowakabili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Emmanuel Mkongo akisaini kitabu cha wageni Shule ya Msingi Kisimiri Juu.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa