Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya ameshiriki Mbio zilizoandaliwa na Taasisi ya Sayansi ya Nelson Mandela ( NM-AIST). Mbio zilizokuwa na lengo la kuhamasisha ushiriki wa watoto wa kike katika masomo ya Sayansi ngazi ya Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu ili kuongeza idadi kubwa ya wanawake waliobobea katika masuala ya Sayansi.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji katika Mbio hizo amehimiza suala la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024 na kuwataka washiriki kufikisha ujumbe huo kwa familia, ndugu jamaa na marafiki ili Watanzania wote wapate Elimu hiyo.
Kupitia Nelson Mandela Marathon Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru na Mkurugenzi Wa Halmashauri Mwl.Zainabu J.Makwinya amepata fursa ya kutoa elimu ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27.11.2024 nchi nzima ukitanguliwa na zoezi la uandikishaji wa wapiga kura katika ofisi za vitongoji kuanzia tarehe 11.10.2024 hadi tarehe 20.10.2024.
Kufuatia elimu hiyo, washiriki wa marathon wameonesha uelewa wao walioupata kupitia elimu hiyo ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kutoa wito kwa Wananchi wote kujitokeza kujiandikisha na kujitokeza kupiga kura siku ya tarehe 27 Novemba 2024.
Akisema hayo mara baada ya marathon, Mhadhiri wa Taasisi ya Nelson Mandela (NM-AIST) Prof.Michael Kisangiri ameshukuru kupata elimu hiyo na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kuchagua viongozi wa ngazi ya chini kabisa wanaozijua vizuri changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao zikiwemo changamoto za barabara, maji, elimu na afya. Naye Prof. Revocatus Machunda pamoja na Bi.Juliana Shikosh ambao wote ni washiriki wa mbio hizi na Wahadhiri katika Taasisi ya Nelson Mandela wameshukuru kupata elimu ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Movemba 27 na kutoa wito kwa watanzania wote kutumia fursa iliyotolewa na Serikali ya kujiandikisha tarehe 11-20 Oktoba na kupiga kura ifikapo tarehe 27 Novemba katika vituo vilivyotangazwa na Serikali.
" Serikali za Mitaa , sauti ya wananchi, jitokeze kushiriki uchaguzi"
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa