Mapema hii Leo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya ameongoza Wananchi, Wadau wa Mazingira pamoja na watumishi mbalimbali katika kuadhimisha Siku ya Usafishaji Duniani
Zoezi lililofanyika katika kata ya Usa-River
Katika zoezi hilo Mkurugenzi Mtendaji amewataka Wananchi kuwa Mstari wa mbele kuhakikisha wanatumza maeneo Yao wanayoishi na maeneo wanayofanyia biashara
Aidha ametoa pongezi na shukrani za dhati kwa Wadau mbalimbali walioweza kujitokeza hususani Abagurusi Foundation Pamoja na Dunia salama ambao wamekuwa Mstari wa mbele Kila linapokuja swala la Usafishaji wa Mazingira pia ametoa pongezi kwa wafanya biashara wa siko la Usa-River kwa namna wanavyozidi kubadilika katika swala zima la utunzaji wa Mazingira hususani katika maeneo Yao ya biashara
Mwisho ametoa wito kwa Wananchi na wafanya biashara kuacha kutumia mitaro kwa ajili yakupitisha Maji machafu badala yake kuhakikisha kuwa Kila mmoja anakiwa na Septic Tank kwa ajili ya Maji taka
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa