Na Annamaria Makweba
Pamoja na kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan inaleta fedha nyingi katika Halmshauri zote Nchini, lakini ni jukumu la kila Halmashauri kutenga bajeti ya Mapato ya Ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali katika maeneo yao.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Meru, Mwl. Zainabu J. Makwinya amefanya Ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.
Kati ya Miradi aliyotembelea ni pamoja na Mradi wa ukarabati wa Maabara katika shule ya Sekondari Mulala iliyopo katika Kata ya Songoro ambayo ilipatiwa fedha kiasi shilingi Milioni 8. Lakini pia, shule ya Sekondari Nkoarisambu iliyopo Kata ya Nkoarisambu iliyopatiwa fedha kiasi cha shilingi Milioni 18 kwa ajili ya ukamilishaji wa Maabara.
Miradi mingine aliyotembelea ni pamoja na ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa shule ya Sekondari Ngorika iliyopo Kata ya Maji ya Chai ambapo walipatiwa kiasi cha fedha shilingi Milioni 30, Shule ya Sekondari Ngurudoto katika Kata hiyo ya Maji Chai ilipatiwa kiasi cha shilingi Milioni 13 pamoja na Ujenzi wa Matundu 15 ya vyoo katika Sekondari ya Muungano iliyopo Kata ya Usariver iliyopewa kiasi cha fedha shilingi Milioni 21.
Mbali na kukagua Miradi hiyo, Mwl. Makwinya amesikiliza kero na changamoto mbalimbali za watumishi katika Kata hizo, kero za majengo kongwe, barabara mbovu, tatizo la upatikanaji wa maji na umeme na kuahidi kuzifanyia kazi kwa haraka na zile ambazo hazitakuwa kwenye uwezo wake ameahidi kuzifikisha kwa wahusika ili zitatuliwe.
Mwl. Joyce Elibariki Elia ni Kati ya waliowasilisha changamoto za walimu kwa Mkurugenzi Mtendaji ikiwa ni pamoja kutopanda daraja ya Mshahara, kutolipwa malimbikizo ya Mshahara pamoja na kutolipwa fedha za uhamisho. Ambapo Mwl. Zainabu ametoa maelekezo kwa shule zote kuchagua mwakilishi wao atakayekusanya changamoto hizo zikiwa na vielelezo vinavyojitosheleza ili viweze kufanyiwa kazi.
Vilevile Mwl. Zainabu ameahidi kufuatilia suala la Mwl. Regina S. Dionis aliyestaafu na kulipwa mapunjo ya mafao yāke na kutolipwa malipo ya kupanda daraja kabla ya kustaafu, ambapo ameelekeza suala hilo kwa Mkuu wa Divisheni ya Rasilimali watu kutatua changamoto hizo.
Katika ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji alifuatana na baadhi ya wataalam kutoka Halmashauri.
Hata hivyo, Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali walikuwepo katika maeneo ambayo yalikaguliwa. Viongozi hao ni pamoja na Wenyeviti wa Serikali ya Vijiji, Wajumbe wa kamati ya Siasa, Waheshimiwa Madiwani pamoja na wananchi.
Kwa nyakati tofauti, Waheshimiwa Madiwani wa Kata zilizotembelewa na Viongozi wa Kamati za Siasa Wamemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaletea Mkurugenzi Mtendaji Mwl. Zainabu J. Makwinya katika Halmashauri ya Meru.
"Shukrani na pongezi kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea Mkurugenzi Jembe na anayefanya kazi kwa bidii, hakika sisi watu wa chama tukitakiwa kusema basi na hili tutalisemea" alisema Omari Salimu Mtali Katibu Mwenezi Kata ya Usariver.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa