Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Emmanuel Mkongo amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu toka kwa Diwani wa Kata ya King'ori ,Ndg Peter Kessy.
Peter Kessy Amewaambia waandishi wa Habari hana budi kuunga mkono juhudi za Mhe .Rais Dkt.John Joseph Pombe Magufuli katika kuwaletea Watanzania maendeleo.
Hata hivyo amejivua uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (C.C.M).
Diwani Peter Kessy ni Diwani wapili kujiuzulu ndani ya Mwezi huu ambapo Tarehe 18 mwezi huu Aliyekuwa diwani wa Kata ya Kikwe Paul Shango aliwasilisha kwa Mkurugenzi barua ya kujiuzulu kwa kile alichodai ni kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya tano.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru inajumla ya Kata 26 hadi sasa jumla ya kata mbili Kikwe na King'ori hazina wawakilishi wa Ngazi ya Udiwani katika Baraza la halmashauri baada ya madiwani wake kujiuzulu nafasi hizo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa