Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Emmanuel Mkongo amethibitisha kupokea barua ya kujiuzulu toka kwa Diwani wa Kata ya Majengo Ndg.Bernard E. Kivundo.
Diwani Bernard Kivondo amesema hawezi kupinga maendeleo yanayotekelezwa kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo amejiuzuli kumuunga mkono Mhe .Rais Dkt.John Joseph Pombe Magufuli katika kuwaletea Watanzania maendeleo.
Hata hivyo amejivua uanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (C.C.M).
Halmashauri ya Wilaya ya Meru inajumla ya Kata 26 hadi sasa jumla ya kata tatu Kikwe na King'ori na Majengo hazina wawakilishi wa Ngazi ya Udiwani katika Baraza la Halmashauri baada ya madiwani wake kujiuzulu nafasi hizo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Emmanuel Mkongo akipokea barua ya kujiuzulu toka kwa Diwani wa Kata ya Majengo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa