Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange ameipongeza halmashauri ya wilaya Meru kwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa jengo la huduma za dharura (EMD) katika hospitali ya wilaya ya Meru mkoani Arusha.
Ametoa pongezi hiyo leo tarehe 10 Machi 2023 baada ya kuridhishwa na ujenzi wa jengo hilo uliogharimu shilingi milioni 300.
Dkt. Dugange ameagiza Halmashauri kukamilisha ujenzi wa jengo hilo ambao upo katika hatua za ukamilishaji na kuhakikisha ifikapo tarehe 20 Aprili 2023 huduma zote zianze kutolewa kikamailifu kwa wananchi.
Amesema kazi zilibaki katika jengo hilo ni pamoja na kufunga mfumo wa gesi ya oxygen, mfumo wa TEHAMA, mfumo wa kiyoyozi na kuweka kingo kwenye ngazi.
Aidha, Dkt. Dugange amesema tayari Serikali imetumia shilingi milioni 438 kununua vifaa tiba vilivyofungwa katika jengo hilo ikiwa ni pamoja na mashine ya kidigital ya X- Ray.
Dkt. Dugange ameiagiza halmashauri kuweka mpango kazi wa haraka wa kukamilisha miradi yote ambayo haijakamilika ili ianze kutoa huduma kwa wananchi.
Kwa Upande wake, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Dkt. Danielson Pallangyo amemshukuru Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ujenzi wa jengo hilo la huduma za dharura.
Dkt. Pallangyo ameiomba Serikali kutenga fedha za kukarabati hospitali ya Wilaya Meru ambayo ni kongwe na baadhi ya majengo yamenza kuchakaaa.
Aidha Katika ziara hiyo Mhe.Naibu Waziri alitembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mareu, Ujenzi wa Zahanati ya Msitu wa Mbogo na Ujenzi wa Jengo la huduma za dharura( EMD) katika Hospitali ya Wilaya ya Meru (TENGERU)
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa