Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na utunzaji wa Mazingira) Mhe. Dkt. Seleman Jafo ameipongeza Wilaya ya Arumeru kwa utunzaji wa Mazingira hususani vyanzo vya maji ambapo ameelekeza Halmashauri za Wilaya hiyo kutenga bajeti zitakazo akisi uhalisia wa utunzaji wa Mazingira.
Mhe.Dkt. Jafo amesema hayo alipotembelea chanzo cha Maji Usa- Spring kilichopo ndani ya msitu wa Nkoanekoli katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru unaosifika kwa kuwa na mbega weupe "niwapongeze Wananchi na Viongozi wa Arumeru kwa utamaduni wa kutunza vyanzo vya maji "amesema Mhe.Dkt.Jafo
Aidha, Mhe.Jafo amesema kwa kutambua umuhimu wa utunzaji wa Mazingira Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameelekeza utunzaji wa mazingira kuwa Agenda ya kudumu " hatuna mbadala wa Suala la utunzaji wa mazingira, tumeanza kushuhudia athari za mabadiliko ya tabia ya nchi, hapa Arusha tunaona kiwango Cha joto kimeongeka ,Pia kwa Mkoa wa Dar es Salaam upatikanaji wa Maji kwa matumizi ya binadamu umepungua, niwasihi tutunze vyanzo hivi" Amehimiza Mhe.Dkt. Jafo
Katika Ziara hiyo ya Mhe.Waziri Dkt. Jafo amekagua uhifadhi wa chanzo Cha Maji Usa- Spring ,ametembelea Kitalu cha Mti cha Halmashauri ya Wilaya ya Meru pamoja na kupanda mti eneo la Midawe Halmashauri ya Arusha.
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na utunzaji wa Mazingira) Mhe. Dkt. Seleman Jafo akizungumza wakati wa ziara katika Wilaya ya Arumeru (kulia )Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi Richard Ruyango.
Ziara ya Mhe.Jafo kukagua chanzo Cha Maji Usa- Spring.
Mtiririko wa Maji katika msitu wa Nkoanekoli kilipo chanzo chanzo cha Maji Usa- Spring
Afisa Maliasili Ndg.Charles Mungure akitoa maelezo kwa Mhe. Waziri Jafo alipotembelea Kitalu cha mti cha Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Miche ya Miti katika Kitalu cha Miche Cha Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Miche ya Miti katika Kitalu Cha Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bangata wameshiri katika zoezi la upandaji miti eneo la Midawe wakati wa ziara ya Mhe Waziri Jafo katika Wilaya ya Arumeru.
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na utunzaji wa Mazingira) Mhe. Dkt. Seleman Jafo akipanda mti katika eneo la Midawe Wilayani Arumeru.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bangata wameshiri katika zoezi la upandaji miti eneo la Midawe wakati wa ziara ya Mhe Waziri Jafo katika Wilaya ya Arumeru.
anafunzi wa Shule ya Sekondari Bangata wameshiri katika zoezi la upandaji miti eneo la Midawe wakati wa ziara ya Mhe Waziri Jafo katika Wilaya ya Arumeru.
Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na utunzaji wa Mazingira) Mhe. Dkt. Seleman Jafo wakati akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bangata Wilaya Arumeru amesema ni wakati wa kila Mwanafunzi kupanda na kutunza mti.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa