Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, amewasili mkoani Arusha na Viongozi ambao ni wenyewe, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda alipowasili kiwanja cha Ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro leo 6 Machi, 2024.
Ujio wa Makamu wa Rais mkoani Arusha ni kwa ajili ya kufungua Mkutano wa 21 wa Taasisi ya Fedha, unaofanyika kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha (AICC) Ukumbi wa Simba.
Mhe. Mpango amemuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo ambaye ndiye mgeni rasmi. Hata hiyo, katika mkutano huo Mada kuu itakayojadiliwa ni kuimarisha ustahimilivu wa Sekta ya Fedha nyakati za changamoto za kiuchumi.