Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Elimu bila Mipaka ( Education Beyond Borders) imetambua Mchango wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru kuwaruhusu walimu kutoka Shule za Sekondari na Msingi Katika Wilaya ya Meru kushiriki Mafunzo yaliyotolewa nchini Kenya.
Mratibu EBB Mwl. Godlizen Z. Kaaya kutoka shule ya Msingi Kisimiri chini kwa niaba ya walimu walioshiriki mafunzo hayo nchini Kenya amewasilisha cheti kwa Afisa Maendeleo ya Jamii Bi. Flora Msilu kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Mwl. Zainabu J. Makwinya.
Mratibu wa EBB Taifa Mwl. Kaaya ameeleza kuwa wamejifunza masuala ya kijamii na hisia (Social and Emotional Learning) na namna ya kukabiliana na changamoto za wanafunzi, walimu na hata wazazi.
" Kati ya Mambo tuliyojifunza ni pamoja na kuangalia hisia za mtoto, mzazi na mwalimu ili kujua namna ya kuzungumza nao wakati wa kuwahudumia hasa mtu akiwa kwenye msongo wa mawazo au hali ya kihisia. " amesema Kaaya.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa