Diwani Viti maalum Tarafa ya Poli (CCM), Mhe.Felista Nanyaro amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kupata kura za ndiyo za Madiwani wote 34 waliohudhuria Mkutano huo.
Akizungumza baada ya wajumbe kupiga kura wakati wa mkutano maalum wa mwaka wa fedha 2021/2022 Mwenyekiti halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe.Jeremia Kishili, amemtangaza Mhe. Felista Nanyaro kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo mara baada ya ya kushinda kwa kura za ndiyo, "tulipokea jina la mgombea mmoja nafasi ya Makamu mwenyekiti wa Halmashauri nimpongeze kwa kupata kura za ndiyo" amesema Mhe. Kishili
Aidha, Mhe. Felista amewashukuru madiwani wenzake kwa kumuamini na kumchagua kushika nafasi hiyo kwa mara ya pili na kuahidi kushirikiana nao pamoja na Mwenyekiti, uongozi mzima wa Halmashauri kwa kuhakikisha mipango na shughuli mbalimbali za maendeleo zinasimamiwa vizuri ili kuendelea kuwaletea wananchi maendeleo.
Vilevile katika uchaguzi huo wenyeviti wa kamati za kudumu walichaguliwa ambapo
Mhe. Essau Sikawa Diwani wa Kata ya Nkoaranga amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira. Mhe. Laurence Ngolly Diwani Wa Kata ya Mbuguni amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji. Mhe. Lukumbwe Ndossi Diwani wa Kata ya Malula amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, na Mhe.Felista Nanyaro Makamu Mwenyekiti atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kudhibiti UKIMWI.
Ikumbukwe Mwenyekiti wa Kamati ya fedha ,Utawala na Mipango ni Mwenyekiti wa Halmashauri.
Mhe.Jeremia Kishili Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mhe.Felista Nanyaro Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
Mhe. Laurence Ngolly Diwani Wa Kata ya Mbuguni na Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji.
Mhe. Lukumbwe Ndossi Diwani wa Kata ya Malula na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya wakati Mkutano.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano.
Waheshimiwa Madiwani wakati wa Mkutano.
Wataalam wakati wa Mkutano.
Wataalam wakati wa Mkutano.
Wataalam wakati wa Mkutano.
Wataalam wakati wa Mkutano.
Wataalam wakati wa Mkutano.
Wataalam wakati wa Mkutano.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa