Tangu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2020 Waheshimiwa Madiwani kuingia madarakani na kuanza rasmi kutekeleza Majukumu yao katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe. Felister Nanyaro Diwani Viti Maalumu Tarafa ya Poli amefanikiwa kugombea na kushinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri.
Kama ilivyoelekezwa kwenye Kanuni za Kudumu za Halmashauri za Sheria ya Serikali za Mitaa ( Mamlaka za Wilaya) (Sura ya 287) sehemu ya 2 kipengele cha 6 (3) kuhusu kufanyika kwa Mkutano wa Kawaida wa Mwaka wa Halmashauri kwamba kutakuwa na ajenda ya Kumchagua Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Kuteua wajumbe wa Kamati za Kudumu, kujadili taarifa ya utendaji na uwajibikaji wa Halmashauri kwa mwaka uliopita pamoja na kupitisha ratiba ya vikao vya Halmashauri.
Wajumbe wamefanya Uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ambapo kati ya Madiwani 35 na Mhe. Mbunge, Madiwani 28 wameshiriki katika zoezi la Uchaguzi na kati ya kura zilizopigwa ni 28 huku Makamu Mwenyekiti Felister Nanyaro kupata kura 27 na kura 1 ya hapana.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa