Tukio hilo lilizinduliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe. Mwinyi Ahmed Mwinyi, ambaye pia alishiriki mbio za kilomita 10 za msituni.
Akizungumza baada ya kumaliza mbio, Mwinyi alisema tukio hilo limechangamsha washiriki kimwili, limeimarisha mshikamano wa kijamii na kuongeza thamani ya utalii wa misitu.
“Ni mbio za kipekee ambazo zimenikutanisha na watu wengi. Changamoto za msitu, maporomoko ya maji na mandhari ya asili yameongeza furaha na msisimko kwa washiriki.
Amewapongeza TFS na waandaaji kwa kuendeleza falsafa ya utalii wa michezo inayosisitizwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa