Halmashauri ya Meru kwa kipindi cha miaka 12 kuanzia( mwaka 2005 hadi 2016 ) ina historia ya kuwa kinara kwenye mashindano ya Kampeni ya Kitaifa ya Usafi wa mazingira inayohusu ujenzi na matumizi ya Vyoo bora na unawaji wa mikono kwa maji tiririka na sabuni.
Historia hii nzurii imetokana na kushika nafasi (tatu bora)mara kwa mara ikipata ushindi kwa nafasi ya kwanza mara 5,nafasi ya pili mara 2 na nafasi ya tatu mara 2 hivyo kupata zawadi mbalimbali ambazo ni Vikombe 6 vya Ushindi ,vyeti vya pongezi pamoja na vifaa ambavyo ni Scanner,Computer Desk Top na Piki piki 2.
Kwa mwaka huu 2017 katika kampeni hizi Halmashauri ya Meru imeongoza kwa asilimia 96 kwa kua mshindi wa kwanza Kitaifa kati ya Halmashauri 185 Tanzania bara zilizoshindanishwa kwenye mashindano haya ya Kampeni ya Kitaifa ya Afya na Usafi wa mazingira yanayohusisha matumizi ya vyoo bora na unawaji wa mikono.
Aidha katika kutekeleza kampeni hiyo kwa upande wa Kijiji bora na Mtaa kwa usafi kiijiji cha Nambala Kilichopo Kata ya Kikwe Kwenye Halmashauri hii ya Meru kilishika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 95.3 huku kijiji cha Kanikale Halmashauri ya Njombe kiishika nafasi ya kwanza kwa kupata asilimia 95.8
Kua Mshindi wa kwanza mwaka huu 2017 Halmashauri ya Meru inatarajia Kukabithiwa zawadi ya Gari aina ya (NISSAN PATROL ) na Pikipiki moja toka Wizara ya( Afya,Maendeleo ya Jamii ,jinsia,wazee na watoo )na pikipiki tarehe 07 Disemba 2017 ,tukio hili litafanyikia Dodoma .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa