Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda amezindua rasmi mafunzo ya Jeshi la Akiba likiwa na jumla ya vijana 128.
Uzinduzi huo umefanyika tarehe 26.07.2023 Viwanja vya Relini Kata ya Usa-river katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru, ambapo Mhe. Kaganda amewapongeza Vijana hao Kwa kuonyesha uzalendo na kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Akiba.
" Ninawapongeza sana kwa uzalendo mliouonyesha kwa kujiunda na mafunzo ya Jeshi la Akiba ,hakika ninyi ni vijana wazalendo na wenye kuipenda Nchi yetu ya Tanzania, ninategemea mnavyoanza mafunzo haya ndivyo mtakavyomaliza msikate tamaa na kuishia njiani ili siku mkimaliza mafunzo yenu tuwashangilie Kwa ukomavu wenu" alisema Mhe. Kaganda.
Aidha, Mkuu huyo amempongeza Binti aliyemaliza digrii ya kwanza ya Ualimu na kuamua kujiunga na Jeshi la Akiba kwani Kwa kufanya hivyo ameonyesha uzalendo mkubwa katika jamii yake na kwa taifa kwa ujumla.
" Vijana walio wengi wanaomaliza Vyuo vikuu wamekuwa na dhana potofu katika masuala la kizalendo kama alivyofanya Binti huyu, hakika amekuwa mfano wa kuigwa na vijana wengine kwani Nchi inahitaji mashujaa wa kuendelea kulinda Uhuru wa Nchi. " Alisema Kaganda.
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amesema mafunzo haya yanafanyika Kwa mujibu wa sheria ya Usalama wa Nchi ( National Defence Act) No . 24 ya mwaka 1966.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa