Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Mhandisi, Richard Ruyango amewataka walimu wa wilaya hiyo kufundisha zaidi wanafunzi sambamba na kuwajenga nidhamu ili waweze kuongeza ufaulu
Mhandisi Ruyango amesema hayo wakati wa hafla ya utoaji motisha chanya na hasi kwa matokeo ya mitihani ya Taifa ikiwemo utoaji wa sanamu za vinyago katika shule zilizofanya vibaya
Akizungumza na walimu hao jana katika halfa ya utoaji wa motisha kwa walimu na shule za Ruyango alisema kuwa endapo walimu hao wakifundisha vema ufaulu wa watoto ikiwemo nidhamu vitakuwepo
Pia. Amesisitiza fedha zilizotolewa na Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan za ujenzi wa madarasa zitumiwe vema ili kuondoa changamoto ya ukosefu wa vyumba vya madarasa katika wilaya ya Meru
Naye Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Meru,Emmy Mfuru amewapongeza walimu hao kwa ufaulu mzuri ikiwemo kushika nafasi mbalimbali kimkoa na kitaifa ikiongozwa na shule ya sekondari ya Kisimiri
Mfuru amesema Halmashauri ya wilaya ya Meru inajumla ya shule za sekondari 66 kati ya hizo shule 37 ni za serikali na shule 29 ni zisizo za serikali ambapo idadi ya wanafunzi 24,186 huku wavulana wakiwa ni 11,576 na wasichana ni 12,607 kwa ujumla .
Vilevile Mfuru ameeleza kuwa wameamua kutoa motisha ya vinyago kwa shule ambazo zimefanya vibaya kuwapa hamasa ya kuongeza ufaulu zaidi na kusisitiza zawadi hizo zitakuwa za mzuunguuko
Hafla hiyo imeenda sanjari na ugawaji wa fedha kwa walimu wa masomo ambayo wanafunzi wamefaulu, Pia na kutoa mchele kilo 25 kwa shule binafsi na za serikali zilizofalisha vema na zawadi ya makombe ya ushindi kwa shule zikizofaulisha
Baadhi ya walimu hao akiwemo,Staraton Shao kutoka shule ya sekondari Ngabobo na Hilda Mally walishukuru kwa zawadi hizo sanjari na kuahidi kutoa ushirikiano kwa wanafunzi ikiwemo ongezeko la ufaulu ili kuondoa aibu kwa baadhi ya shule zilizoambulia vinyago .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa