Leo tarehe 25 Oktoba, 2024 Halmashauri ya Wilaya ya Meru imefanya kikao cha Tathmini ya Lishe Wilaya kujadili taarifa za robo ya kwanza kwa mwezi Julai hadi Septemba 2024.
Mwenyekiti wa Kikao Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Amir Mkalipa ametoa maelekezo kwa Watendaji wa Kata kuhakikisha shule zote zinaunda Klabu za Lishe ikiwa ni pamoja na kuwataka Watendaji hao kuhakikisha Mhe. Mkuu wa Wilaya anaalikwa kwenye Mikutano ya wananchi kwenye Kata ambazo zinachangamoto ya kuchangia chakula shuleni ili aweze kuzungumza na wazazi.
"Nataka Shule zote katika Wilaya ya Meru ziwe na Klabu za lishe ili elimu hii iweze kuwafikia kwa karibu, lakini hakikisheni mnanialika kwenye mikutano ya wananchi inapofanyika kwenye maeneo yenu ili niweze kuzungumza na wazazi ambao hawachangii chakula shuleni. " amesema Mkalipa.
Afisa Lishe Wilaya Asia Ijumaa amewasilisha taarifa ya Utekelezaji ikionyesha hali ya Lishe Ngazi ya Vituo vya kutolea huduma za Afya ambapo kwa Halmashauri ya Meru yenye jumla ya watoto Chini ya miaka mitano 41,075 kwa Mujibu wa Sensa ya Mwaka 2022, watoto 40,884 sawa na asilimia 99.5 wamepimwa hali ya Lishe kwa kutumia kiashiria cha Uzitou na Umri.
Aidha, ametoa pongezi kwa Watendaji wa Kata kwa kazi nzuri wanazofanya kwani wameendelea kutoa elimu ya Lishe katika maeneo mbalimbali , pia wameweza kuwafika wananchi zaidi ya 17,728 kwa wiki ya unyonyeshaji Duniani.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa