Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa Arusha Denis Msiye ameeleza kuwa programu ya mradi wa mzazi hodari imefanya vizuri kwa Halmashauri 3 za Mkoa wa Arusha ambazo ni Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Halamshauri ya Wilaya ya Arusha na Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.
Amesema hayo kwenye kikao kazi cha Tathmini ya utekelezaji wa mradi wa mzazi hodari unaotekelezwa na shirika la Girl Effect, kikao kilichofanyika Hotel ya Mount Meru Leo tarehe 13 Septemba 2024.
Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Arusha wameshiriki kikao hicho akiwemo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Ndg . Seleman Msumi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Karatu Ndugu Juma Mussa Hokororo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa