Halmashauri ya Wilaya ya Meru imeadhimisha siku ya upandaji miti kwa kupanda miti elfu 5 kwenye chanzo cha maji cha Mto ndurumanga Leganga .
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe.Idd Kimanta ambaye ni mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya upandaji miti kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru amepongeza juhudi za Halmashauri hiyo kwenye upandaji na utunzaji wa miti pamoja na utunzaji wa mazingira na kuiagiza kuhakikisha miti iliyopanda inalindwa na kutunzwa ili iendelea kukua.
Mhe.Kimanta amemwagiza Afisa Maliasili wa Halmashauri hiyo kusimamia sheria ili kuhakikisha misitu pamoja na vyanzo vya maji vinalindwa ipasavyo.
Afisa maliasili wa Halmashauri hiyo Charles R. Mungure amesema kwa msimu wa mvua wa Julai hadi Disemba 2017 jumla ya miche ya miti laki 686,000 ilipandwa na katika msimu huu Ofisi ya Mkurugenz Mtendaji wa Halmashauri hiyo imesambaza jumla ya miche elfu 51 kwenye Kata zake na Vijij na zoezi hilo la usambazaji na upandaji miti linaendelea ili kufikia lengo la taifa kwa kila Halmashauri kupanda Miti milioni 1.5 kwa kipindi cha mwaka mmoja.
PICHA ZA TUKIO.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Idd Kimanta akipanda mti wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji mti kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt.Aman Sanga akiandaa mti kwaajili ya kuupanda wakati wa upandaji mti kwenye Chanzo cha maji cha mto Ndurumanga
Afisa maliasili wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Charles R. Mungure akipanda mti wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji mti kwenye Halmashauri hiyo.
Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakiwa kwenye harakati za kupanda mti wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji mti kwenye Halmashauri hiyo.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Meru Mukzin Zikatimu akijiandaa kupanda mti wakati wa maadhimisho ya upandaji mti katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Afisa maendeleo ys jamii kutoka Bonde la Pangani amesema majukumu yao ni pamoja na usimamizi vya maji juu na chini ya ardhi pia kulinda na kuzuia uchafuzi na kuhakikisha maji yanapatikana hivyo ni wadau walio mstari wa mbele kwenye suala zima la mazingira
Tito Kitomari ambaye ni mwenyekiti wa umoja wa watumia maji Kikuletwa amesema upandaji mti huo ni ujumbe kwa jamii kuwa vyanzo vya maji vinnatakiwa kutunzwa.
Emmanuel Judica ambaye ni mwanafunzi wa Darasa la 7 katika shule ya Msingi Nshupu akidhibitisha utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila mtu .
Samweli W. Kinga ambaye ni mwananchi mkazi wa kitongoji Cha Makadirisho kinachopakana na chanzo cha maji cha Mto Ndurumanga ametoa wito kwa wananchi wengine kuacha shughuli zote zinazoleta uharibifu wa vyanzo vya maji na uaribifu wa mazingira .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa