KUTOKA WILAYANI ARUMERU.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mkoani Arusha imeshika nafasi ya 6 kitaifa kati ya Halmashauri na Manispaa 195 kwenye matokeo kidato cha nne kwa mwaka 2018.
Halmashauri hiyo imeendelea kuongoza kwenye Mkoa wa Arusha kwa kushika nafasi ya kwanza matokeo ya kidato cha nne 2018 huku ikifuatiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bwn.Emanuel Mkongo amewapongeza waalimu wakiongozwa na mkuu wa idara ya elimu Sekondari Mwl.Damari Mchome kwa ufundishaji na usimamizi mzuri wa maswala ya Elimu .
Mkongo ameeleza kuwa Halmashauri hiyo imeweka mikakati ya kuboresha swala la Elimu ikiwa ni pamoja na agenda ya mimba za utotoni kuwa ya kudumu kwenye mikutano ya vijiji na Kata.
Aidha Mkongo ametoa wito kwa jamii na wadau wa elimu Kushiriki kuboresha Sekta ya Elimu hususani katika ujenzi wa Miundombinu (Mabweni, Madarasa, Maabara, Vyoo, Nyumba za Walimu na Ofisi za Walimu) kwenye Halmashauri hiyo.
Akipokea pongezi kwa niaba ya walimu, Afisa Elimu Sekondari kwenye Halmashauri hiyo amewapongeza wasichana kwa kuongoza kwenye matokeo hayo.
Matokeo hayo ya Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha nne uliofanyika mwaka 2018 yametangazwa rasmi mjini Dodoma na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Dkt Charles Msonde.
Kuona matokeo ya kidato cha Nne 2018
http://www.tamisemi.go.tz/app/form_4_results_2018/results/p0418.htm
Kuona Mpangilio wa Halmashauri/Manispaa kwa ubora wa ufaulu CSEE2018 bofya hapa
https://cdn.necta.go.tz/files/Mpangilio_wa_HalmashauriCSEE2018.pdf
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa