Mwenyekiti wa Halmashauri ya meru Bw. Willy Njau amesema ushirikiano na umoja uliopo ndio umepelekea Halmashauri Mkupata hati safi katika ukusanyaji wa mapato.Akizungumza na waandishi wa habari katika halmashauri hiyo muda mfupi baada ya kuhitimisha kikao cha baraza Bwana Njau amesema kuwa Halmashauri hiyo imefanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia 98 ambapo wamevuka lengo lililokusudiwa .
Bwana Njau amesema mbinu zilizotumika hadi kufikia lengo hilo ni pamoja na timu ya ukusanyaji wa mapato kuwa nzuri ambapo wameonyesha ushirikiano katika zoezi la ukusanyaji huku akisema kuwa mwaka Jana walikusanya kwa asilimia 87 jambo ambalo amesema kwa mwaka wa fedha 2016/17 wamefanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia 98.
Amesema kiwango cha serikali kilichopangwa ni asilimia 80 ili Halmashauri kuweza kupata ruzuku kwa asilimia 100 kutoka serikali kuu ambapo amesema Halmashauri hiyo imevuka lengo kwa kukusanya zaidi ya asilimia 98.
Amesema wamejipanga kwa mwaka wa fedha wa 17/ 18 kuhakikisha wanakusanya mapato zaidi ambapo amesema ili kufikia lengo husika wanaboresha kamati ya fedha na pia kuhamasisha zaidi wananchi katika swala la ulipaji kodi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa