HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU YAADHIMISHA SIKU YA WAJANE DUNIANI.
Kufuatia kauli mbiu isemayo " IMARISHA MIFUMO YA NISHATI SAFI ILI KUKUZA UCHUMI WA WAJANE NA FAMILIA"
Halmashauri ya Wilaya ya Meru imethibitisha kauli mbiu hiyo kwa kuwakutanisha wajane kwa pamoja kuwapatia Elimu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mheshimiwa Jeremiah Kishili awataka wanawake kuinuka na kukataa kauli ya mpaka wawezeshwe ndo wanaweza.
Mhe. Kishili amezungumza hayo wakati wa kufungua Hafla ya Wajane Duniani iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Muungano Usa-river na kuwataka wanawake kuinuka na kujiwezesha na kufanya kazi Kwa bidii.
Aidha Mhe. Kishili ameonyesha umuhimu wa kuwepo kwa Wataalamu wa saikolojia na wanasheria kwani wanawake wanapaswa kufahamu haki zao na jinsi yakuweza kupata haki hizo.
Vilevile, Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya Bi. Flora Msilu amewataka wanawake wajane kufuatilia fursa mbalimbali zinazotolewa katika Halmashauri kama vile mikopo ya asilimia 10 ambayo inaanza kutolewa mwezi wa 7, 2024.
Diwani wa Viti Maalum Kata ya Mbuguni Mheshimiwa Husna Maganga awataka wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali kuelekea kwenye uchaguzi kuanzia ngazi ya Serikali za Mitaa na baadaye uchanguzi Mkuu.
Hafla iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka Taasisi binafsi na Serikali.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa