Shule ya Sekondari Kisimiri ,iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru ,Wilayani Arumeru yashika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya kuhitimu kidato cha Sita mwaka 2020 ambapo wanafunzi wote walio hitimu wamefaulu kwa kupata daraja la kwanza (Division one).
Shule hii imeshika Nafasi ya kwanza kitaifa kwa mara mbili mfululizo na imekuwa katika nafasi kumi za kwanza kitaifa (top ten) kwa kipindi cha miaka 10 mpaka sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Emmanuel J. Mkongo amewapongeza Idara ya Elimu kwa usimamizi na Walimu wa Shule hiyo kwa uwajibikaji wenye tija pia amesema mafanikio hayo ni matokeo ya utendaji shupavu wa Serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi shupavu wa Mhe. Dkt.John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania "nawapongeza sana Walimu washule ya Sekondari Kisimiri kwa utendaji wenye tija"amesema Mkongo.
Mkuu wa shule hiyo .Mwl.Valentine Tarimo amesema siri ya kufanya vizuri kwa Shule hiyo ni ushirikiano wanaoupata kuanzia ngazi ya Wilaya sambamba na Walimu Kufanya kazi kwa kujituma pia shule hiyo imeweka mpango wa kufanya vizuri kitaalum kwa kuwa na mkakati ,utekelezaji wa Mikakati na usimamizi makini .
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa