Mkuu wa Divisheni ya Rasilimali watu na Utumishi Halmashauri ya Wilaya ya Meru Edward Bujune ametoa salamu za Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya ambapo katika salamu hizo amewapongeza Walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya Ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Bujune ametoa Pongezi hizo wakati wa tamasha la kuwapongeza walimu na kutoa motisha Kwa walimu Kwa kazi nzuri wanayoifanya lililoandaliwa na Idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Meru Leo Tarehe 25 Julai 2024.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa