• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

Jamii yaaswa kuhakikisha wajawazito wanawahi kufika katika vituo vya huduma za afya ili kuepusha vifo na madhara kwa watoto wachanga.

Imewekwa: January 8th, 2021

Jamii  yaaswa kuhakikisha wajawazito wanawahi kufika katika vituo vya huduma za afya ili kuepusha vifo na madhara kwa watoto wachanga.

Akizungumza wakati wa kikao cha  kujadili vifo vitokanavyo na Uzazi na kujifungua katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt.Jackline Urio ambaye ni Daktari  bingwa wa Magonjwa ya watoto kutoka hospitali ya rufaa ya Mkoa ya Mt.Meru amesema kuna uwezekano mkubwa mtoto kuzaliwa akiwa na uharibifu wa selihai za ubongo na kupelekea ulemavu wa kudumu pia kupoteza maisha endapo mama mjamzito atachelewa kufika katika kituo cha kutolea huduma za afya kwa wakati.

Dr. Urio  ametoa wito kwa jamii kuachana na dhana potofu ya mama mjamzito kusubiri hadi hatua ya kujifungua ndipo aelekee hospitali kwani ni miongoni mwa sababu za vifo vya mama wajawazito na watoto  "kinamama acheni dhana ya kusubiri uchungu wa kujifungua ndipo uelekee kituo cha kutolea huduma za afya" amehimiza Dkt.Urio

Aidha Dkt.Urio amefafanua kuwa kuwahi katika vituo vya huduma kuna imarisha afya ya mama na pia uwezekano mkubwa wa wataalamu wa afya kuweza kuokoa maisha ya watoto wachanga pamoja na mama .

Mwakilishi wa Mganga Mkuu Mkoa wa Arusha Bi. Vones Uiso amesema Serikali katika kudhibiti vifo vitokanavyo na uzazi  imeanzisha mpango wa kuhakikisha viongozi wa ngazi ya jamii wanashirikishwa kwa karibu katika swala zima la kujadili huduma za afya.

viongozi ngazi  kijamii wamepongeza ushirikishwaji wao na kutoa wito kwa baadhi ya wananchi ambao ni wakunga wajadi wasio na  mafunzo ambao hawajatambuliwa kwa taratibu za afya  wanaochangia  kinamama wajawazito kujifungulia majumbani   kuacha kwani serikali itawachukulia hatua kwa kuhatarisha maisha ya kinamama .

Ndugu Ten ambaye ni Afisa   Tarafa ,Tarafa ya Mbuguni amesema kuna umuhimu mkubwa wa elimu ya afya ya uzazi hivyo  wataalamu wa afya afya ngazi ya Kata kushirikiana na Wilaya hawana budi kutoa elimu ya kina kuhusiana na afya ya uzazi.

Naye Mratibu wa afya ya Uzazi katika Halmashauri ya Meru Bi. Sikudhani Mkama amesema  pamoja na kupungua kwa vifo vya kina mama kutoka 6 mwaka 2019 hadi 1 mwaka 2020 bado idadi ya  vifo vya watoto chini ya miaka 5 imeongezeka kutoka 34 mwaka 2019 hadi 41 mwaka 2020.

 Pia. Mratibu huyo amesema  kunauwezekano mkubwa wa idadi hiyo kuongezeka kwani   mwenendo wa viashiria vya hali ya afya ya uzazi  hususani Kiashiria cha idadi ya wanaojifungulia vituoni   ni asilimia 58% ambapo ni chini ya lengo la kitaifa,"tuwahimize kinamama wajifungulie vituo vya huduma kuepuka vifo vya watoto wachanga"amesisitiza Sikudhani.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dr Maneno Focus amewataka waganga wafawidhi katika vituo vya kutolea huduma kuzingatia maagizo yanayotolewa na viongozi mbalimbali ikiwemo kusimamia huduma kwa weledi na maadili ili kuleta tija kwenye utoaji wa huduma za afya,  Pia.kusimamia mapato na kuinua viashiria muhimu vya huduma kwa zaidi ya asilimia 20 katika robo ya mwaka januari hadi machi 2021.

Aidha Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Meru kikiwajumuisha kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT).Maafisa Tarafa,wadau wa afya  na watendaji wa kata, kilifunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Ndg.Jerry Muro ambaye aliwataka maafisa tarafa, Watendaji waVijiji na  Kata  sambamba na  Viongozi wa Idara ya afya kuhakikisha wanahimiza wananchi kujiunga na Mfuko wa bima ya afya ya jamii ulioboresha ICHF ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa huduma bora za afya.

  Daktari  bingwa wa Magonjwa ya watoto Jackline Urio.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt. Maneno Focus


Wajumbe wa kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT)

 Mratibu wa afya ya Uzazi katika Halmashauri ya Meru Bi. Sikudhani Mkama

Wajumbe wa kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT)

Afisa Tarafa Mbuguni Bw. Abdalah Teni akizungumza wakati wa kikao .

Wajumbe wa kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT)

Wajumbe wa kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT)


Wajumbe wa kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT)


Wajumbe wa kamati ya uendeshaji afya wilaya(CHMT)


Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa