Halmashauri ya Meru imeungana na mataifa mengine , kuadhimisha wiki ya Unyonyeshaji Dunia, kwa kuikumbusha jamii umuhimu wa unyonyeshaji maziwa ya mama kwa watoto wachanga na lishe bora kwa mama anayenyonyesha .
Akizungumza katika wiki ya unyonyeshaji iliyonza tarehe 01 hadi 07 Agosti Kaimu Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Stela Maya ametoa wito Kwa wanawake kunyonyesha watoto wachanga kwa kipindi cha miezi sita bila kuwaanzisha vyakula vingine kwani maziwa ya mama hutoa virutubisho vyote ambavyo mtoto mchanga anahitaji na kuwalinda kutokana na magonjwa na maambukizi mbalimbali ambapo amehimiza baada ya miezi sita mtoto ataendelea kunyonyeshwa kwa miaka miwili au zaidi.
Aidha Maya amesema watoto ambao hawanyonyeshwi katika miaka ya kwanza ya maisha wana uwezekano mkubwa wa kushambuliwa nw magonjwa.Pia ameeleza mama anayenyonyesha, anapaswa kula makundi matano ya vyakula ili kupata virutubisho vya kutosha wakati wa unyonyeshaji, ambavyo huwezesha mwili wake kutengeneza na kutoa maziwa ya kutosha kadri mtoto anavyohitaji.
Miongoni mwa kina mama waliohudhuria elimu katika wiki ya unyonyeshaji wamesema ni muhimu kwa kinamama kuwapa watoto haki yao ya kunyonya ili watoto kukua vizuri "wamama tunyonyeshe tuwasaidie watoto wetu kukua vizuri na kuwa na afya nzuri "amehimiza Ndeshifose Mkazi wa Malula
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa