• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

MATUMIZI YA UZAZI WA MPANGO WAUNGWA MKONO NA UWIRO NA NGABOBO

Imewekwa: December 13th, 2017

Wananachi wa Kata ya Uwiro na Ngabobo waunga mkono matumizi ya Uzazi wa mpango ili kutoa malezi bora kwa watoto na kuboresha  Afya ya Mama ,hili limedhihirishwa na  wawakilishi toka kata hizo ambao ni wenyeviti wa Vijiji, wajumbe wa Serikali za vijiji, viongozi wa kimila, viongozi wa kiroho, wakunga wa jadi, viongozi wa vijana na kinamama na baadhi ya Wanachi , baada ya kupata  semina juu ya matumizi ya mpango wa uzazi na umuhimu wa mama mjamzito ambaye mimba itaharibika kusafishiwa hospitali pamoja na umuhimu wa kujifungulia Hospitali, kwenye Semina ya Matumizi ya uzazi wa mpango iliyotelewa  imetolewa na wahudumu wa afya wa jamiii waliopewa mafunzo na shirika la Engender Health ambao ni Elizabeth Richard na Piterson N. Nnko iliyofanyikia katika Kituo cha Afya cha Ngarenanyuki  tarehe 13 Disemba 2017.

Aidha wawakilishi hao  wamepongeza uwepo wa semina hiyo iliyofadhiliwa na Shirika la Engender Health kwa kushirikia na Halmashauri ya Meru  na kutoamsimamo kua  wataelimisha na kuwahamasisha wananchi wengine ambao hawajapata fursa hii ya kuhudhuria semina hiyo kutumia njia za uzazi wa mpango, sambamba  wanawake wajawazito kujifungulia kwenye Hospitali (vituo vya Afya) pamoja na wajawazito ambao  mimba zitaharibika kuhakikisha wanapata huduma ya kusafishwa kizazi kwenye Hospitali.

Martha Yakobo ambaye ni Mkunga wa Jadi amesema baada ya kupata elimu kupitia semina hiyo  kwa sasa atakua mstari wa mbele kuhamasisha kina mama wajawazito kujifungulia Hospitalini  kwa usalama wao na usalama wa mtoto atakayezaliwa pia atawashauri wanawake kutumia uzazi wa mpango ili kuboresha malezi kwa watoto na Afya ya mama.

Salome J. Mbegela ambaye ni Mratibu wa Uzazi wa mpango kwenye Halmashauri ya Meru  ameitaka jamii hiyo kuondokana na mtizamo hasi kuhusu matumizi ya uzazi wa mpango kwani hauna madhara yoyote kwani yeye binafsi ameutumia kwa zaidi ya miaka 20  pia ametoa elimu juu ya njia zote za uzazi wa mpango na kueleza umuhimu wa kutumia vituo vyaa  afya kupata huduma mbalimbali ikiwemo kujifungua.

Salome J. Mbegela ambaye ni Mratibu wa Uzazi wa mpango kwenye Halmashauri ya Meru  akieleza umuhimu na faida za kutumia uzazi wa mpango


Sebastian A. Macrice ambaye ni mratibu wa shirika la Engender Health  akihimiza mama mjamzito anapoharibikiwa na mimba kuhakikisha anasafishwa kizazi kwenye Hospitali(kituo cha Afya)


Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa