Jamii imehimizwa kuwasaidia kina mama kuwanyonyesha watoto wachanga maziwa yao pekee bila kuwapa vyakula vingine kwa kipindi cha miezi 6 ya mwanzo kwani maziwa ya mama yanavirutubisho muhimu ambavyo humkinga mtoto dhidi ya magonjwa hatarishi kama vile kuhara , magonjwa ya hewa na maskio.Pia maziwa ya mama ni kinywaji na chakula kinacho msaidia mtoto kukuwa vizuri kimwili na kiakili,hayo yamejiri katika Kilele cha maadhimisho ya wilki ya onyonyeshaji katika Halmashauri ya Meru, Wilayani Arumeru yaliyofanyika Hospitali ya Wilaya .
Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt.Maneno Focus amesema maziwa ya mama ni muhimu sana kwani huwa na protini zote, vichochezi vya ukuzi, mafuta, wanga, vimeng’enya na vitamini ambavyo ni muhimu kwa ukuzi wenye afya wa Mtoto mchanga katika miezi ya kwanza ya maisha hivyo amewahimiza kina mama kunyonyesha watoto maziwa yao pekee kwa miezi 6 na pale wanapofika umri kuanzia miezi 7 mbali na kuwa mtoto anaweza tumia vyakula vya lishe wanatakiwa kuendelea kuwanyonyosha hadi wafike umri wa miaka miwili kwakuwa katika kipindi hicho ndipo ubongo wa mtoto hujitengeneza.
Aidha Dkt.Maneno ametoa rai kwa jamii kuwasaidia kina mama kunyonyesha maziwa yao pekee miezi 6 ya mwanzo kwa kuacha dhana ya kuamini mtoto hashibi maziwa ya mama bali kuwajengea mazingira ya kupata maziwa ya kutosha kwa kuwapa lishe stahili pamoja na faraja ili kumwondolea msongo wa mawazo.
Aidha Dkt.Maneno amehitimisha kwa kufafanua kuwa iwapo jamii itashiriki kikamilifu kumsaidia mama kunyonyesha miezi 6 ya mwazo itasaidia kupunguza na kumaliza lishe duni kwa mtoto kwani takwimu zinaonyesha hali ya udumavu Mkoani Arusha ni asilimia 25.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Meru Dkt.Maneno Focus akizungumza wakati wa kilele cha Wiki ya unyonyoshaji.
Familia yaBw.Daniel Eliasi
Kinamama wakifuatilia mafunzo ya unyonyeshaji.
Afisa Lishe Halmashauri ya Meru Asia Ijumaa,amesema kunafaida wapatazo kinamama wanaonyonyesha kwani kwa asilimia kubwa kunyonyesha hupunguza kupata ugonjwa wa saratani ya matiti pia humsaidia mama kurejea kwenye maumbile yake ya awali kabla ya kupata ujauzito.
Kinamama wakipata elimu juu ya unyonyeshaji maziwa ya Mama.
Afisa Lishe akijibu swali la Mama alihoji nini kifanyike endapo mama hana maziwa ya kutosha? Swali hili limejibiwa endapo itatoke mama anachangamoto ya kunyonyesha afike katika kituo cha Afya kilichopo karibu ili apewe huduma na ushauri wa kitaalamna
Ndg.Daniel Elias ameeleza yeye humsindikiza mkewe kwani ni jukumu lao wote kumlea mtoto,pia ni faraja kwa Mama na humfanya mtoto kuhisi anapendwa na wazazi wote.
Katika Kilele cha Maadhimisho yaWiki ya unyonyeshaji elimu imetolewa juu ya unyonyeshaji maziwa ya mama,ulaji bora wa vyakula pamoja na upimaji magonjwa yasiyoambukiza na ushauri wa kitaalamu umetolewa katika viguo vyote vya Afya vya Halmashaur ya Meru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa