Uongozi wa Kijiji cha Imbaseni waiomba Serikali kusajili Shule ya Sekondari iliyoanzishwa na Wananchi wa Kijiji hicho ambapo wamejenga vyumba Vinne vya Madarasa vilivyofikia hatua ya lenta.
Uongozi huo imetoa ombi hilo wakati WA hafla ya uzinduzi wa madawati 40,Meza mbili na Viti katika Shule ya Msingi Imbaseni,ambapo Mhe.Jeremia Kishili Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru amezindua madawati hayo na kupongeza jitihada hizo za Uongozi wa kijiji kutumia rasimali miti iliyopandwa eneo la Shule kutengeneza madawati na kuhimizwa kuendelea kupanda miti.
Aidha, Mhe.Kishili amesema Halmashauri itaungamkono ujenzi Wa vyumba Vinne vya Madarasa vya Shule ya Sekondari ambavyo vimejengwa na Wananchi kufikia hatua ya lenta.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel Mkongo ametoa wito kwa Viongozi wa vijiji vingine kuiga mfano wa kutumia rasilimali zilizopo kutatua changamoto na kuharakisha Maendeleo katika maeneo hayo.
Mkongo amepongeza Uongozi wa Kijiji Cha Imbaseni kulipa kipaombele Swala la Elimu ambapo mbali na kutatua changamoto katika Shule ya Msingi wameanzisha ujenzi Wa Shule ya Sekondari.
Mkongo amesema ujenzi Wa vyumba Vinne vya Madarasa ni miongoni mwa miundo mbinu muhimu hivyo ameshauri Uongozi huo kukamilisha miundombinu mwingine kama vile Maabara,vyoo na Ofisi ya walimu
Mhe.Jeremia Kishili Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru akizindua madawati katika Shule ya Msingi Imbaseni.
Madawati mapya yaliyotengenezwa na Uongozi wa Kijiji Cha Imbaseni.
Ujenzi Wa Vyumba Vinne vya Madarasa katika Shule mpya ya Sekondari kijiji Cha Imbaseni ambapo Uongozi wa kijiji hicho umeiomba Serikali kuisajili.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa