Halmashauri ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kichama Meru imepongeza namna Serikali ilivyowaletea maendeleo wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ikiwa ni utekelezaji wa ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015.
Akizungumza wakati wa Mkutano huo ,Katibu wa CCM Wilaya ya kichama Meru Ndg. Gurisha Mfanga amesema Chama cha Mapinduzi kipo imara na kinaendelea kuisimamia Serikali kuwaletea wananchi maendeleo ambayo yamefanyika Meru na yanaendelea kufanyika na kuwavutia zaidi Wananchi na viongozi mbalimbali kuendelea kuiamini CCM chini ya uongozi makini wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amesema Serikali chini ya uongozi makini wa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, imeboresha Sekta ya elimu kwa kwa kutoa zaidi ya Milioni 100 kwaajili ya elimu bila Ada kila mwezi katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Muro amesema Serikali imeboresha Miundombinu ya madarasa,nyumba za walimu na maabara za kujifunzia masomo ya sayansi hivyo kuwezesha Halmashauri hiyo kufanya vizuri kwa kushika nafasi ya tatu Kitaifa na nafasu ya kwanza kimkoa katika matokeo ya mtihani wa Taifa wa kidato cha nne na kidato cha pili kwa mwaka 2019.
Aidha,Muro amewaeleza Wajumbe wa Halmashauri ya CCM Wilaya kuwa Shule ya Sekondari Kisimiri uliyopo Meru imeshika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2019.
Akihitimisha Muro amesema katika Sekta ya afya Serikali imesogeza huduma karibu na wananchi kwa kutoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujezi ujenzi na ukarabati wa kituo cha afya Usa -River ambacho kwa sasa huduma mbali mbali zinatolewa ikiwemo ya upasuaji .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel J. Mkongo amesema Halmashauri hiyo kupitia wataalamu wake itaendelea kutekeleza shughuli za Serikali kwa uadilifu na kuendana na kasi ya Mheshimiwa Rais inayolenga kuwaletea maendeleo wananchi hususani wanyonge.
Aidha, Mkutano huo wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya kichama Meru umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambapo umeridhia utekelezaji wa ilani ya CCM katika Wilaya ya Kichama ya Meru .
Katibu wa CCM Wilaya ya kichama Meru Ndg. Gurisha Mfanga.
Wajumbe wa Halmashauri ya CCM Wilaya ya Kichama ya Meru.
Katibu wa CCM Wilaya ya kichama Meru Ndg. Gurisha Mfanga.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro akisoma ilani ya chama cha mapinduzi CCM
Wajumbe wa Halmashauri ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kichama Meru wakati wa Mkutano.
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel J. Mkongo akizungumza wakati wa Halmashauri kuu ya CCM.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Ndg.Emmanuel J. Mkongo
Wajumbe wa Halmashauri ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kichama Meru wakati wa Mkutano.
Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Wakuu wa Idara na Vitengo Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Mkuu wa Idara ya Utawala na rasilimali watu Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa