Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango, Halmashauri ya Wilaya ya Meru wameanza ziara ya siku mbili ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo, kufuatia Sheria, Kanuni na Taratibu za serikali za mitaa, inayoitaka Kamati hiyo ya Fedha kukagua miradi kila baada ya miezi mitatu katika mwaka wa fedha husika.
Aidha, ziara hiyo inatoa fursa kwa wajumbe wa Kamati hiyo kuweza kukagua na kutoa mapendekezo ya Miradi ya Maendeleo inayo tekelezwa na Halmashauri kwa kipindi husika.
Miradi inayokaguliwa ni ya kipindi Cha robo ya nne, kwa Mwaka wa fedha 2020/2021
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa