Kamati ya Mpango Mkakati wa kupambana na kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto Halmashauri ya Wilaya ya Meru (MTAKUWWA), imetakiwa kuwa balozi wa kutoa elimu ya kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto kwa kutekeleza vyema mkakati wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwani kumekuwa na matukio mengi ya ukatili wa kijinsia katika jamii.
Rai hiyo imetolewa na Mhe.Felister Nanyaro, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru wakati akifungua Mafunzo ya siku tatu kwa wajumbe wa Kamati ya mpango Mkakati wa kupambana na kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto (MTAKUWWA ) ngazi ya Wilaya.
Aidha mafunzo hayo yataendelea kwa siku tatu katika ukumbi wa Halmashauri ambapo wajumbe wa MTAKUWWA ngazi ya Wilaya toka makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini pamoja na wataalam mbalimbali wameshiriki.
Mafunzo hayo yamefsndiliwa na Shirika la SOS TANZANIA
https://www.instagram.com/p/CgRQPKUND_K/?igshid=MDJmNzVkMjY=
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa