• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

KAMATI YA SIASA WILAYA YA KICHAMA MERU YARIDHISHWA NA UJENZI UNAOENDELEA WA ZAHANATI YA KIJIJI CHA ILIKIRIMUNI.

Imewekwa: February 4th, 2020

Kamati ya Siasa Wilaya ya kichama ya Meru, Meru  imeridhishwa na mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Ilikirimuni Kata ya Ngarenanyuki Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kueleza kuwa Serikali kupitia Arusha National Park(ANAPA) imetekeleza vyema Ilani ya uchaguzi ya CCM ibara ya 50 inayoielekeza Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi wake katika umbali mdogo.

Haya yamejiri Siku ya Kwanza ya ziara ya kamati hiyo kwenye Halmashauri ya Meru ambapo Katibu  wa CCM Wilaya ya Meru Ndg. Gurisha Mfanga  amepongeza hatua za ujenzi wa zahanati hiyo yenye thamani ya Shilingi Milioni 125,285,805 ikiwa kiasi cha Milioni 87,700,063.50 ni fedha kutoka ANAPA na Shilingi Milioni 37,585,741.50 ni michango ya Wananchi. Pia ameielekeza Halmashauri kupeleka huduma  ambazo zinaweza kutolewa wakati ukamilishaji unaendelea  na kuhoji  mchango wa Halmashauri kwenye ujenzi huo ikizingatiwa ni Kata ya pembezoni.

Akitoa ufafanuzi Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Ndg. Emmanuel J Mkongo  ameahidi kufanyia kazi maelekezo ya Chama na kueleza kuwa kwa mwaka wa fedha uliopita  2018/2019 kila Kata ilipewa Shilingi Milioni kumi kwaajili ya miradi ya Maendeleo ikiwepo Kata ya Ngarenanyuki pia Halmashauri imehakikisha Mradi huo unajengwa kwa viwango kupitia Mhandisi wa ujenzi .

Naye Mheshimiwa diwani wa Kata ya Ngarenanyuki Zacharia Nnko kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Ngarenanyuki hususani Kijiji cha Ilikirimuni ameishukuru Halmashauri kwa ufunguzi wa barabara kuelekea kituoni hapo "ufunguzi wa barabara hii ni mwangaza kwa zahanati hii kwani bila Halmashauri kuleta mtambo na kufungua barabara hii tusingeweza kufika hapa leo hii"Amefafanua Mhe.Zacharia

Katibu tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.James Nchembe ametoa wito kwa Viongozi wa Kata na Vijiji  kuwajengea uelewa wananchi ili waweze kuchangia ujenzi wa miradi ya maendeleo "sisi sote ni watanzania hatuna budi kujiletea maendeleo kwa kuchangia ujenzi wa  mradi huu wa afya maendeleo hayana mipaka " amesisitiza Mwl. James

Aidha ziara hiyo imekamilika kwa siku ya kwanza kwa Kukagua Mradi wa ujenzi wa Kijiji cha Ilikirimuni na Jengo la  Wodi ya Mama na Mtoto katika Zahanati ya kijiji cha Kwaugoro ambapo Chama  kimeielekeza Halmashauri kuongeza idadi ya Watumishi katika zahanati ya Kwaugoro sambamba na Watumishi wa zahanati hiyo kuhakikisha kunakwepo na usafi wa kuridhisha .

Jengo la Zahanati ya Ilikirimuni.

Mtendaji wa Kijiji cha Ilikirimuni akitoa ufafanuzi wakati wa ukaguzi.

Ukaguzi jengo la zahanati Ilikirimuni.

Katibu wa CCM akitoa maelekesho  ya kutoa huduma za afya katika Jengo la Zahanati ya Ilikirimuni.


Mkurugenzi Mtendaji Halmashairi ya Wilaya ya Meru akizungumza wakati wa ukaguzi wa Jengo la Zahanati ya Ilikirimuni.


Katibu tawala Wilaya ya Arumeru akizungumza wakati wa ukaguzi wa Jengo la Zahanati ya Ilikirimuni.



Kamati ya siasa ikiwa katika Zahanati ya Kijiji cha Kwaugoro.

Jengo la mama na mtoto katika Zahanati ya Kijiji cha ilikirimuni.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kichama Meru ,Ndg.Gurisha Mfanga.



Katibu tawala Wilaya ya Arumeru Mwl.James Nchembe akisisitiza uzalendo kwa Watumishi wa Zahanati ya Kwaugoro.

Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa