• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

KAMPENI YA JIONGEZE TUWAVUSHE SALAMA YAZINDULIWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MERU.

Imewekwa: July 25th, 2019

Kampeni ya jiongeze tuwavushe Salama imezinduliwa katika Halmashauri ya Meru, Wilayani Arumeru ambapo mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Arumeru,Mhe.Jerry Muro, amesema Wilaya hiyo itasimamia vyema Kampeni hiyo inayolenga kupunguza vifo vya mama wajawazito pamoja na watoto wachanga, hivyo jamii na watoa huduma za afya wanapaswa kutekeleza wajibu wao kwa wakati "kuwa mjamzito  na kujifungua si ugonjwa hivyo kinamama na watoto ni lazima wawe salama kwani uhai ni haki yao"amesisitiza Mhe Muro.

Aidha Muro amemwagiza Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dkt.Maneno Focus Kuwakumbusha watoa huduma za afya kutekeleza wajibu wao kwa weledi pia kutumia lugha zenye staa na rafiki kwa wagonjwa sambamba na kuacha matumizi ya simu za mkononi yasio muhimu wakati wa saa za kazi "kauli nzuri kwa mgonjwa humpa faraja na kuwa sehemu ya tiba" amefafanu Muro.

Mganga Mkuu Dkt.Maneno Focus amesema Serikali imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuhakikisha dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma vinakuwepo ambapo kwa Halmashauri hiyo hali ya uwepo wa dawa muhimu wakati wa kujifungua ni zaidi ya asilimia 98.

Aidha  Dkt. Focus  aliainisha kuwa katika kipindi cha mwezi Januari hadi Juni mwaka 2019 kumekua na vifo  viwili vitokanavyo na uzazi ingawa bado kuna changamoto ya upatikanaji wa taarifa sahihi toka kwenye jamii ambao hawafiki kwenye vituo vya kutolea huduma, hivyo kampeni hiyo inalenga kuongeza uwajibikaji kwa viongozi wa dini, siasa, kijamii na wadau wote kuwajibika na kuhakikisha  vifo vya uzazi vinadhibitiwa.

Naye Mratibu wa Kampeni hiyo ngazi ya Halmashauri Ndg.Sikudhani Mkama amesema Halmashauri imeweka mikakati ya kuhakikisha utekelezaji wa kampeni ya jiongeze tuwavushe salama inafanikiwa na ametoa rai kwa  jamii na familia kutimiza wajibu wao ili kupunguza na kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi.

Akizungumza kwa niaba ya wadau wa Afya Philomena Marijan toka Shirika la kimataifa lisilo laSerikali DSW ambalo huwawezesha vijana kwa kuwajengea mazingira wezeshi pamoja na kuongeza ushiriki wao katika ma swala ya afya ya uzazi,uchumi na uongozi, ameipongeza Halmashauri hiyo  kulipa kipau mbele swala la afya ya vijana na elimu juu ya afya ya uzazi.

Aidha uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri umekamilika kwa maafisa Tarafa  kula kiapo cha usimamizi wa utekeleza wa Kampeni hiyo.

PICHA ZA TUKIO

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Jiongeze tuwavushe Salama.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Meru Dkt.Maneno Focus.


Kiongozi wa Mila ,Mzee wilson Kaaya,Mshili mkuu ukoo wa Kaaya akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya jiongeze tuwavushe Salama.

Philomena Marijani toka Shirika la kimataifa lisilo laSerikali DSW akizungimza kwa niaba ya wadau wa afya.

Picha ya pamohja Meza kuu na wadau wa Afya.



Mhe.Diwani kata ya Akheri (wa kwanza kulia) Viongozi wa Dini na Mila wakati wa uzinduzi.

Watumishi wa Idara ya Afya wakati wa uzinduzi .

Wakuu wa idara Halnashauri ya Meru wakati wa uzinduzi

Wadau wa Afya









Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO WIKI YA UTYUMISHI WA UMMA 2025 DODOMA

    June 13, 2025
  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa