Wakuu wa Shule za Sekondari zinazotekeleza miradi ya vyumba vya Madarasa 70 katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru wameushukuru Uongozi wa Halmashauri kwa kurahisisha upatikanaji wa vifaa vya ujenzi ikiwemo Saruji, mbao na bati " vifaa hivi vimeharakisha utekelezaji wa miradi hii ikizingatiwa ni mingi na uhitaji ni mkubwa" amesema Mwl.Hasan Rajabu Mkuu wa Shule ya Momela
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Mwl.Zainabu Makwinya amesema Halmashauri hiyo imeweka mikakati ya kuhakikisha vyumba hivyo 70 vya madarasa vinakamilika kwa wakati ambapo baada ya kutoa Saruji na miradi mingi kufikia hatua ya ufungaji Lenta na upauzi , tayari mbao za upauzi wa Miradi hiyo zimewasili, na bati zilishapatikana.
Mwl.Makwinya ametoa wito kwa Wakuu wa Shule, wataalam pamoja na Viongozi wa maeneo miradi inapotekelezwa, kuendelea kushirikiana ili miradi hiyo kukamilika kwa wakati na kuwa na tija iliyokusudiwa na Serekali ya awamu ya Sita inayo ongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan.
Ikumbukwe,Serikali ya awamu ya Sita ilitoa Shilingi Bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 70 vya Madarasa katika shule za Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru , fedha hizi ni za mkopo wa riba nafuu kutoka shirika la fedha Duniani,ikiwa ni Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO -19.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya alipokuwa akitoa maagizo juu ya utekelezaji wa miradi ya vyumba 70 vya Madarasa, mara baada ya Halmashauri kuhakikisha uwepo wa Saruji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru baada ya kuhakikisha vifaa/bati zinapatikana, zoezi la ugawaji bati kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya vyumba 70 vya Madarasa katika shule za Sekondari lilifanyika.
Mbao zitakazotumika kwenye ujenzi miradi ya vyumba vya Madarasa 70 katika Shule za Sekondari zikiwa zimewasili katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
Saruji ilipowasili.
Maendeleoya ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa Shule ya Sekondari Lakitatu
Maendeleoya ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa Shule ya Sekondari Nshupu
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa