Katibu Mkuu ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Eng.Joseph Nyamhanga, alipotembelea mradi wa Chumba cha darasa Katika Shule ya Msingi Ndoombo Halmashauri ya Meru Wilayani Arumeru ambao umekamilishwa kwa fedha za mradi wa lipa kulingana na matokeo EP4R, amesema Serikali kwa Mwaka wa fedha 2018/2019 imetoa Bilioni 65.4 kwaajili ya ujenzi na ukamilishaji wa miundombinu ya elimu Nchini ambapo Bilioni 29.9 zilitolewa kukamilisha miundombinu Shule za Sekondari na Bilioni 35.5 zilitolewa kukamilisha miundombinu shule za Msingi, pia imetoa Bilioni 288.485 kwaajili ya Elimu bure ili kuhakikisha watoto watoto wote wa kitanzaniawenye umri wa kwenda shule wanakwenda bila Kero ya ada na kudaiwa michango.
Aidha Eng.Joseph Nyamhanga, ameridhishwa na ubora wa ujenzi wa darasa hilo katika shule ya Msingi Ndoombo uliokamilishwa kwa milioni 12.5 fedha toka Serikalini za programu wa EP4R ambao nguvu za wananchi na mchango wa Halmashauri ulifikisha Darasa hilo hatua ya Lenta , amepongeza ufuatiliaji na usimamizi wa fedha za Uboreshaji wa Miundombinu ya Elimu Wilayani hapo.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru,Emmanuel Mkongo ameishukuru Serikali ya awamu ya Tano kwa kuboresha Miundombinu ya Elimu katika Halmashauri hiyo kwani mwaka wa fedha 2018/2019 imepokea Zaidi ya milioni 300 kwaajili ya ujenzi wa vyumba 4 vya madasa,matundu 12 ya choo katika Shule za Msingi Tanzanite na Kisimiri juu na ukamilishaji wa maboma 16(vyumba vya madarasa )katika shule 16 za Msingi sambamba na utoaji wa fedha za Elimu bila malipo kila mwezi, ambapo Halmashauri hiyo hupokea Zaidi ya milioni 60 kugharimia elimu bure kwa shule za Sekondari pia hupokea zaidi ya milioni 55 kwaajili ya Elimu bure shule za Msingi.
Mkongo ameeleza Elimu bure imeleta mafanikio makubwa katika Halmashauri, kwani kunaongezeko kubwa la idadi ya wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza na Darsa la awali ,mwaka 2015 wanafunzi waliojiunga na kidato cha kwanza walikuwa 2622 na 2018 wakawa 4484, pia 2015 waliojiunga na darasa la awali walikua 6809 na 2019 ni 7700.
Mkongo amesema kwa kiasi kikubwa Elimu bure imeongeza ufaulu ambapo matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi darasa la saba ( vii ) mwaka 2015 asilimia ya ufaulu ilikua 67.6% na 2018 ikawa 86.6%,pia katika mtiani wa Kuhitimu kidato cha nne mwaka 2015 asilimia ya ufaulu ilikua 95.7% na mwaka 2019 ni 99.4% .
Katibu mkuu Eng.Joseph Nyamhanga,anaendelea na ziara yake Katika Wilaya ya Monduli MKoani Arusha.
Katibu mkuu ofis ya Rais TaAMISEM akizungumza ndani ya chumba cha darasa Shule ya Msingi Ndoombo kilichokamilishwa kwa fedha za P4R milioni 12.5
Katibu Mkuu ofisi ya Raisi TAMISEM akizungumza baada ya kukagua chumba cha Darasa Shule ya Msingi Ndoombo.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakati wa Ziara.
Wakuu wa Idara na Vitengo wakati wa Ziara
Vyumba vya Madarasa vilivyoboresha kupitia programu ya EP4R shule ya Msingi Tanzanite.
Matundu ya Choo shule ya Msingi Tanzanite
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa