Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesikiliza kero za wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Kata ya Usariver akiwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na kusikiliza kero za wananchi katika Halmashauri hiyo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi balozi Daktari Nchimbi, ametoa maelekezo mbalimbali kwa viongozi kuhakikisha kero zote za wananchi zinatatuliwa na kufanyiwa kazi kwa wakati.
Katika ziara hiyo, Dkt . Nchimbi ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Komredi Amos Gabriel Makalla na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Hamid Abdalla.
Balozi Dkt. Nchimbi amemaliza ziara yake kwa Mkoa wa Arusha kuelekea Mkoa wa Kilimanjaro.
|
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa