Katibu Tawala Wilaya ya Arumeru Joseph Mabiti mapema hii Leo tarehe 08 Februari 2025, amefungua kikao cha Tathimini ya Lishe ya Wilaya kujadili robo ya pili Oktoba hadi Desemba 2024 kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Meru akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Amir Mohamed Mkalipa .
Katika kikao hiko Mabiti Amewataka Watendaji wa Kata kuwasimamia Watendaji wa Vijiji katika kuhakikisha ulaji wa chakula kwa watoto mashuleni linasimamiwa kwa ufanisi Mkubwa ili kuleta Maendeleo kwa watoto walioko mashuleni na kuhakikisha wanapata lishe Bora.
Aidha, katika uwasilishaji wa Taarifa ya Tathimini ya lishe Kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba 2024 Kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Meru Asia Juma Amesema kuwa Swala la lishe Kwa upande wa Meru liko katika kiwango cha juu Kwa asilimia 95.1 huku kiwango cha Chini cha Lishe kikiwa Ni asilimia 1.0 aidha amefafanua na kusema juhudi za kufanikisha swala la lishe kuwa Bora nikutokana na Elimu wanazotoa kupitia Nyanja mbalimbali na kwa ushirikiano wa idara mbalimbali ikiwemo idara ya Maendeleo ya Jamii.
Pia, katika kikao hicho Elimu juu ya umuhimu wa viini Lishe vilivyopo kwenye mboga, Viungo na Matunda imetolewa kupitia Mseminishaji Happy Saanya ambapo ametoa Elimu juu ya zao la Selery huku akionyesha umuhimu na Faida zitokanazo na zao hilo.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa