Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yawakutanisha Wadau mbalimbali kujadili utekelezaji wa upangaji wa ARUSHA AFCON CITY eneo linalotarajiwa kujengwa Uwanja wa AFCON Mkoani Arusha.
Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano katika Hoteli ya Ngurdoto na kufunguliwa na Ndugu Deogratius Kalimenze Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi na kuhudhuriwa na Wadau kutoka Taasisi mbalimbali ikiwemo TANESCO, TARURA, TANROAD, RUWASA na wengine.
Aidha, Wataalamu wa Idara za Ardhi kutoka Halmashauri za Mkoa wa Arusha wameshiriki kikao hicho huku lengo la kikao hicho likiwa nikujadili namna Bora ya upangaji na uendelezaji wa Mji huo unaotarajiwa kuwa na uwanja utakaotumika katika michuano ya AFCON.
kikao hicho kimeondoka na maadhimio yatakayokwenda kuboresha upangaji na uendelezaji wa Mji huo.
Mwisho kikao hiko kimefungwa na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani Tanzania ndugu. Hamduni Zaharan Mansour.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa