Mkuu wa idara ya Afya,Lishe na Ustawi Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt. Evarist Chiweka ameongoza kikao kazi cha Waganga wafawidhi na waratibu wa Afya ngazi ya Halmashauri kujadili Taarifa ya utekelezaji Robo ya pili ya Mwaka 2024-2025. Aidha Dkt. Chiweka katika kikao hiko amewataka Waganga wafawidhi kusimamia majukumu Yao hasa katika kuhakikisha Wananchi wanapata huduma kama inavyostahili Kwa kutumia taaluma zao na namna walivyo aminika na Serikali. Aidha amesisitiza swala la kuendelea kutoa Elimu Kwa Jamii kuhusu umuhimu wa Bima ya Afya na kutoa Elimu na hamasa Kwa wakina Mama wajawazito kuanza kliniki mapema ili kuepusha matatizo wakati wakujifungua na matatizo Kwa Mtoto alie tumboni.
Kikao hiko kimeuzuriwa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya ambae amewataka Waganga hao kusimamia vizuri swala la Mapato kwani Mapato yanapokuwa mazuri itasaidia utoaji wa huduma Bora kwenye Vituo wanavyofanyia kazi, nakusisitiza swala la nidhamu mahali pakazi kama nyenzo Imara ya kudumisha upendo katika Maeneo ya Kazi na kusaidia kuleta tija Kwa Wananchi tunao wauhudumia
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa