Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Meru, Mwl. Zainabu J. Makwinya akizungumza kwenye kikao kazi cha Mkoa wa Arusha cha kupitia Majibu ya Hoja za Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) za mwaka wa fedha 2022/2023, kikao kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kikao hicho kimewakutanisha Wakurugenzi wa halmashauri zote za Mkoa wa Arusha na watendaji wao pamoja na Menejimenti ya Mkoa wa Arusha, kwa lengo likiwa ni kupitia na kujiridhisha na utekelezaji wa Hoja hizo kabla ya kuziwasilisha kwa Mdhibiti na Kkaguzi wa Hesabu za Serikali na kufanya uhakiki.
Katika kikao hicho, Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Mussa, amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Arusha kufanya kazi kwa ushirikiano na upendo na Watendaji wengine ili kutoa majibu ya hoja za ukaguzi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa