Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda akiwa kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arusha - AICC, kwa ajili ya kuongoza kikao kazi cha watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Taasisi za Umma na Mamlaka za Serikali za Mitaaa za Mkoa wa Arusha leo Aprili, 2024.
Mhe. Makonda amesikiliza taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali kutoka kwa Wakuu wa Taasisi za Umma na Serikali za Mitaa na kusisitiza mambo yafuatayo:- Kufanya Tathmini na kuona namna ya Kusafisha Mji kwa kuwatumia Jeshi (JKT) ambapo watafanya usafi watasimamia usafi na utunzaji wa mazingira lakini watashughulikia wahalifu/ Vibaka wanaopora mali za watu.
Aidha, ameelekeza kupitia upya Master Plan ya jiji la Arusha na kuweka mpango bora wa upangaji wa Mji na upangaji wa maeneo ya Viwanja vya Michezo. ambapo amewataka TARURA, RUWASA, TANESCO kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kukubaliana na miundombinu ipi itangulie kuwekwa kabla ya nyingine ili kusitokee uharibifu na kusababisha hasara.
Vilevile, Makonda ameelekeza suala la uwekaji wa Taa za Barabarani zenye ubora kuendana na Hadhi ya Jiji la Arusha ikiwa ni pamoja na kuondoa mabango yasiyokuwa na tija na kuona uwezekano aina moja ya mabango ya Kidigitali ili kuepukana na wingi wa mabango katika maeneo ya Jiji.
Hata Hivyo Mkuu wa Mkoa huyo, amesisitiza suala la kufanya kwa ushirikiano na kupendana ili kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa taifa.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa