Halmashauri ya Wilaya ya Meru Kwa kushirikiana na Shirika la World Vision, TAHA na Farm Concern wametoa Mafunzo ya Siku mbili Kwa kikundi cha Wakulima wa Shambarai Burka na Kerikeny ( SHAMKERI ) kilichopo katika kijiji cha Shambarai Burka Kata ya Mbuguni kinachojishughulisha na kilimo cha Umwagiliaji.
Aidha Mafunzo hayo yalikuwa na Lengo la kusikiliza changamoto wanazokutana nazo wakulima hao, kutoa mbinu mbalimbali za kilimo,kutoa na kuonyesha fursa zinazopatikana masokoni na usimamizi bora wa kikundi Kwa kuzingatia katiba ya kikundi Kwa kufanya marekebisho ya katiba.
Afisa Maendeleo ya Jamii Martha Nardo ametoa ufafanuzi wa uwajibikaji wa Vikundi, Taasisi na Serikali ambapo kwa upande wa Halmashauri ameeleza namna Halamshauri inavyowajibika katika utekelezaji wa upatikanaji wa ruzuku kwa vikundi, usimamizi wa vikundi na kutatua changamoto.
Kati ya Changamoto zilizoibuliwa na Wakulima ni ukosemefu wa Umeme wa TANESCO kwani sola zina zotumika kwa sasa hazina uwezo wa kusukuma maji kwenye matenki ya Umwagiliaji pamoja na miundombinu ya barabara kuwa mibovu
Diwani Kata ya Shambarai Burka Mhe. John Mollel amewatoa hofu wakulima kuhusu suala la umeme kwani ameshirikiri katika kikao cha TANESCO ambapo aliwasilisha changamoto hiyo na kuahidiwa kuwa suala hilo litafanyiwa kazi.
Kupitia Mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya Flora Msilu ameeleza kuwa lengo la kukutana ni pamoja na kuchukua changamoto zitakazowasilishwa kwa viongozi wengine wa Serikali ili kutoa ushirikiano na kutatua changamoto zinazowakabili Wakulima hao, pia kutoa usaidizi wa kina pindi wanapohitaji msaada.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa