• Barua pepe |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
Meru District Council
Meru District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Meru

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Afya
      • Maji
      • Mipango, Takwimu na Ufatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Utumishi na Utawala
      • Usafi na mazingira
      • Ardhi na Maliasili
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo,Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Tehama
      • Manunuzi na ugavi
      • Uchaguzi
      • Sheria
  • Fursa za Uwekezaji
    • Misitu
    • Ufugaji wa Ngombe wa Maziwa
    • Ujenzi wa Kituo cha Biashara
    • Ujenzi wa Eneo la Mapumziko
    • Ujenzi wa kituo cha Mabasi cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Malori cha kisasa
    • Ujenzi wa kituo cha Michezo
    • Kilimo cha Nyanya
    • Ufugaji wa Nyuki
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • AIDS
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Miongozo
    • Fomu mbalimbali
    • Utaratibu
  • Kituo cha habari
    • Maktaba ya Picha
    • Video
    • Habari

DC KAGANDA ATOA MAELEKEZO KWA MAAFISA UGANI KUWASILISHA TAARIFA KILA MWEZI.

Imewekwa: August 29th, 2024

Na. Annamaria Makweba

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Emmanuela Kaganda amewataka Maafisa Ugani kuwa na Madaftari  yanayoonyesha kazi wanazozifanya katika kila Kata na Vijiji.

Mhe. Kaganda ametoa maelekezo hayo leo tarehe 29 Agosti, 2024 katika hafla fupi ya kugawa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani  wa Kata zote 26 za Halmashauri ya Wilaya ya Meru.

"Kila ifikapo mwisho wa mwezi nataka nipate taarifa ya kazi mnazozifanya kwa kila Afisa Ugani. Kila Afisa Ugani awe na Daftari linaloonyesha ameenda Kata au Kijiji gani, amekutana na nani, na huduma gani ameitoa kwa mwananchi huyo" Amesema Kaganda.

Katika zoezi la ugawaji wa vitendea kazi hivyo, Mkuu wa Seksheni ya Kilimo Bi. Digna Massawe ameeleza kuwa mnamo tarehe 10 Agosti 2024, katika Mkutano uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Mhe. Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan aligawa Vitendea kazi kwa Maafisa Ugani wote nchini na Halmashauri ya Meru imepatiwa Vishikwambi 34 na Magwanda 31 kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakulima.

Bi. Massawe ameeleza kuwa lengo la vitendea kazi hivyo ni kwa ajili ya kuboresha huduma za ugani na kuongeza tija ya uzalishaji kwa wakulima wadogo na kuinua kipato chao.

Pia, ameeleza wameandaa mfumo maalum utakaotumika kwenye Vishkwambi ambao  utawasaidia Maafisa Ugani kupiga picha na kuandaa taarifa za huduma wanazotoa,  mahali na muda wa huduma hizo kutolewa.  Hii itasaidia katika kufuatilia maendeleo ya kilimo na kuongeza uzalishaji kwa kutumia teknolojia.

Katika Hatua nyingine Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mhe. Jeremia Kishili amewataka Maafisa Ugani hao kwenda kufanya kazi kwa ushirikiano kati ya Wataalam wa Kilimo na Mifugo hasa katika matumizi ya vitendea kazi vinavyotolewa na Serikali ili kuleta ufanisi kwa kazi zao.

Afisa Ugani wa Kata ya Seela Sing'isi, Ndg. Spora Mtari, ametoa shukrani kwa Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kuona umuhimu wa kuwapa vitendea kazi maafisa ugani ili waweze kufanya kazi kwa weledi na kufikia matarajio ya viongozi na wananchi. Ameahidi kuwafikia wakulima na kuwasaidia kuongeza uzalishaji na utunzaji wa chakula.


Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya ametoa Shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiangalia Sekta ya Kilimo, Mifumo na Uvuvi . Aidha alikumbusha kuwa mbali na kupokea vifaa hivyo mwaka 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Meru ilipokea Pikipiki 29 za maafisa ugani ili kutekeleza majukumu yao.



fungua hapa kupata video,☝️






Matangazo ya Kawaida

  • KUITWA KWENYE USAILI October 28, 2024
  • KUITWA KWENYE USAILI June 24, 2024
  • KALENDA YA UTEKELEZAJI WA MTAALA WA ELIMU YA AWALI NA MSINGI 2022. February 18, 2022
  • UUZAJI WA VIWANJA ENEO LA NGURUDOTO LIMEANZA. November 27, 2018
  • Tazama Vyote

Habari Mpya

  • AJIRA MPYA MERU DC WAPATIWA MAFUNZO

    April 02, 2025
  • NAIBU WAZIRI MAENDELEO YA JAMII,JINSIA WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUMU AKAGUA MIRADI YA S.O.S

    March 15, 2025
  • MAFUNZO YA MFUMO WA TAUSI MERU DC YAFUNGWA

    February 15, 2025
  • TAHAPAO NA MERU DC WAWEKA NGUVU KWENYE KAMATI ZA MTAKUWA

    February 19, 2025
  • Tazama Vyote

Video

ELIMU YA KUKABILIANA NA TAHADHARI YA MVUA ZA EL NINO YAANZA KUTOLEWA HALMASHAURI YA MERU.
Video Zaidi

Viungo Haraka

  • Kupata Salary Slip
  • Sheria ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Meru

Kiungo Kuhusiana

  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Utumishi
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya Mkoa wa Arusha
  • Ajira Portal
  • Government Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Counter

Ramani ya Mahali

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya ya Meru

    Anwani: P.o. Box 462 Usa River

    Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@merudc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa