Kilele cha Mashindano ya kukuza stadi za KKK ,yaani kusoma ,kuandika,kuhesbu, kuchora na utambuzi wa Mwalimu Mahiri katika utengenezaji zana za kufundishia na kujifunzia kwa shule zote za Msingi yamefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa kushiriksha Walimu watano toka shule za kawaida na walimu watano toka shule zenye vitengo vya elimu maalumu, wanafunzi 40 toka shule za kawaida na wanafunzi 10 toka shule zenye vitengo vya Elimu maalumu.
Afisa Taaluma Msingi Halmashauri Wilaya ya Meru ,Mwl.Enock Sangova amesema Serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha wanafunzi wote wanaoingia darasa la tatu wanajua kusoma kuandika na kuhesabu,ambapo ilitoa mafunzo endelevu ya kuwajengea uwezo walimu wa madarasa ya awali ,darasa la kwanza na la pili Nchi Nzima kwa awamu.Katika kuendeleza mafunzo hayo, Ofisi ya Rais TAMISEMI imeanzisha mashindano ya kukuza stadi za KKK yaani kusoma ,kuandika,kuhesbu, kuchora na utambuzi wa Mwalimu Mahiri katika utengenezaji zana za kufundishia na kujifunzia kwa shule zote za Msingi za Serikali Tanzania Bara yakiwa na lengo tajwa hapo juu.
Aidha kilele cha mashindano hayo ni baada ya kufanyika mashindano ngazi za Shule ,Kata ,na Klasta kuanzia 16 Septemba 2019 hadi tarehe 02 Octoba 2019 kwa kushindanisha walimu mahiri na wanafunzi katika ngazi tajwa.
Akifungua Mashindano hayo yaliyoshirikisha Klasta 5 Leganga, Kikatiti, Ngarenanyuki ,Leguruki na Mbuguni, Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri Grace Solomoni ambaye ni mkuu wa Idara ya Kilimo ,Ushirika na Umwagiliaji amewapongeza walimu kwa namna wanavyowajibika kwa kujituma na kufanikisha utoaji wa elimu bora .
Naye Mwenyekiti wa jopo la waamuzi wa mashindano hayo ambaye pia Mthibiti Mkuu wa ubora Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Onesmo Oletaipa wakati wa kutangaza matokeo, amewapo ngeza Walimu na wanafunzi walioshiriki mashindano hayo kwani wameonesha umahiri mkubwa,pia ameeleza katika Halmashauri ya Meru ongezeko nikubwa la wanafunzi wanaojua Kusoma ,Kuandika na Kuhesabu KKK kwa wastani wa asilimia 97%.
Mwl Oletaipa amemtangaza Mwl Neema Kaya toka Shule ya msingi Tuvaila kuwa ni mshindi wa kwanza nafasi ya mwalimu mahiri kwa shule za kawaida, akifuatiwa na Mwl.Nangaiwa Mmbugu toka shule ya msingi Usariver, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mwl Mwanaidi Juma toka shule ya Mwakeny.
Kwa upande wa Shule zenye vitengo vya elimu maalumu Mwl Agnes Kimaro toka shule ya Elimu maalum Patandi kitengo cha wasioona aliibuka mshindi wa kwanza nafasi ya mwalimu mahiri, akifuatiwa na Mwl.Rosemary Killenga toka shule ya Msingi Chemchem kitengo cha elimu maalumu kitengo cha ulemavu wa akili huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Mwl.Anna Shayo toka Shule ya Msingi Elimu maalum Patandi kitengo cha Viziwi.
Matokeo ya Wanafunzi wa darasa la kwanza shule za kawaida, Naomi Paulo toka shule ya Nkoanrua, Klasta ya Leganga aliibuka mshindi katika mahiri ya Kuhesabu, Mwanafunzi Rodney William toka shule ya Ambureni, Klasta ya Leganga aliibuka mshindi katika mahiri ya Kuandika, Mwanafunzi Alpha Evarist toka shule ya Chemchem, Klasta ya Kikatiti aliibuka mshindi katika mahiri ya Kuchora na Mwanafunzi Faith Lain toka shule ya Maasai Vision, Klasta ya Ngarenanyuki aliibuka mshindi katika mahiri ya Kusoma.
Kwa upande wa wanafunzi wa kawaida darasa la pili, Mwanafunzi Glory Zakayo toka shule ya Ulong’a, Klasta ya Leganga aliibuka mshindi katika mahiri ya Kuhesabu, Mwanafunzi Dorini Mkonyi toka shule ya Ngyeku, Klasta ya Kikatiti aliibuka mshindi katika mahiri ya Kuandika, Mwanafunzi Nancy Elisante toka shule ya Tengeru, Klasta ya Leganga aliibuka mshindi katika mahiri ya Kuchora, na Mwanafunzi Innocent Kumbuael toka shule ya Nkoanrua, Klasta ya Leganga aliibuka mshindi katika mahiri ya Kusoma.
Kwa upande wa wanafunzi wenye uhitaji maalum darasa la kwanza, Mwanafunzi Kelvine Mathias toka shule ya Patandi, Klasta ya Leganga aliibuka mshindi katika mahiri ya Kuhesabu na Kuandika kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia, Mwanafunzi Rehema Msitiri toka shule ya Patandi, Klasta ya Leganga aliibuka mshindi katika mahiri ya Kusoma na Kuchora kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia, Mwanafunzi Harison Emmanuel toka shule ya Patandi, Klasta ya Leganga aliibuka mshindi katika mahiri ya Kusoma na Kuandika kwa wanafunzi wenye ulemavu wa uoni hafifu na Mwanafunzi Hashimu Abdi toka shule ya Tuvaila, Klasta ya Kikatiti aliibuka mshindi katika mahiri ya Kusoma kwa wanafunzi wenye ulemavu wa akili.
Kwa upande wa wanafunzi wenye uhitaji maalum darasa la pili, Mwanafunzi Hagai Benedict toka shule ya Patandi, Klasta ya Leganga aliibuka mshindi katika mahiri ya Kuhesabu na Kuandika kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia na Mwanafunzi Ian Sirikiael toka shule ya Patandi, Klasta ya Leganga aliibuka mshindi katika mahiri ya Kusoma na Kuchora kwa wanafunzi wenye ulemavu wa kusikia.
Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha Klasta tano, Klasta iliyoibuka kidedea na kupata ushindi wa jumla ni Klasta ya Leganga.
BAADHI YA PICHA ZA TUKIO.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri Grace Solomoni ambaye ni mkuu wa Idara ya Kilimo ,Ushirika na Umwagiliaji akizungu wakati wa wa kilele cha mashindano ya kukuza stadi za KKK.
Walimu na wanafunzi wakati wa ufunguzi wa Kilele cha Mashindano ya kukuza stadi za KKK.
Mwalimu wa elimu Maalumu akitumia lugha ya alama wakati wa ufunguzi Kilele cha Mashindano ya kukuza stadi za KKK.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri Grace Solomoni ambaye ni mkuu wa Idara ya Kilimo ,Ushirika na Umwagiliaji akipokea maelezo toka kwa ,Mwl.Anna Shayo toka Shule ya Msingi Elimu maalum Patandi kitengo cha Viziwi wakati wa kilele cha mashindano ya kukuza stadi za KKK.
Mwl.Anna Shayo toka Shule ya Msingi Elimu maalum Patandi kitengo cha Viziwi akieleza maana ya lugha za alama .
Mwl Agnes Kimaro toka shule ya Elimu maalum Patandi kitengo cha wasioona akielezea matumizi na maana ya nukta nundu kwa wanafunzi wasiona wakati wa mashindano ya kukuza KKK.
Mwl Agnes Kimaro toka shule ya Elimu maalum Patandi kitengo cha wasioona akielezea matumizi ya kompyuta maalum kwa wanafunzi wenye uoni hafifu wakati wa mashindano ya kukuza KKK.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa