Na Annamaria Makweba
Maadhimisho ya Kilele cha Siku 16 za kupinga Ukatili wa Kijinsia yamefanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Meru huku Mwenyetiki wa UWT Wilaya Julieth Maturo akiwa mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo.
Akizungumza na kundi la wanawake na viongozi mbalimbali katika maadhimisho yaliyofanyika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Muungano, Mwenyekiti huyo ameeleza kuwa Suala la ukatili wa kijinsia ni janga la Dunia nzima.
“ Ukatili wa kijinsi ni janga la Taifa na Dunia nzima, hivyo sisi kama viongozi iwe ni viongozi wa Chama, Serikali na Dini ni jukumu letu kuhakikisha tunapaza sauti kupinga na kukemea ukatili wa kijinsi katika jamii yetu. Alisema Maturo.
Aidha, ameeleza kuwa, UWT imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inapinga masuala yaukatili katika jamii lakini changamoto iliyopo ni wanaofanyiwa ukati li hawatoi ushirikiano ili wahusika wapelekwe kwenye vyombo vya sheria.
Hata hivyo, Mwanaidi Mahanyu kwa niaba ya Afisa Ustawi Mkoa wa ukatili wa kijinsia ambapo ameelezatoa ufafanuzi wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambapo ameeleza kuwa siku hizo zimetokana na mfululizo wa matukio ya ukatili yaliyotokea kuanzia tarehe 10 hadi 25 mwezi disemba miaka ya 1960 ambapo wanawake wengi waliuwawa kikatili katika Nchi za Dominika wakiwa katika harakati za kupinga kunyanyaswa. Hii ikapelekea mwaka 1991 kuanzisha siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia.
Sambamba na ufafanuzi huo, Mahanyu ametoa rai kwa wanawake kupambana kutafuta fedha lakini kupambana zaidi kulea familia kwani mwanamke ndiye mlezi mkuu wa familia.
Pia, Katika maadhimisho hayo, Mwenyekiti UWT amezindua Jukwaa la Uwezeshaji wanawake kiuchumi katika Kata ya Usariver.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Meru Florah Msilu ameeleza kuwa Uzinduzi wa Majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ni Agizo la Serikali,hivyo utekelezaji utafanyika kwa Kata zote 26 na hadi Sasa uzinduzi wa majukwaa hayo umefanyika katika Kata 4 ,Kata ya Kikatiti, Akheri, Ambureni na Usariver. Vilevile ameeleza kufikia mwaka 2024 watazindua Jukwaa la Wilaya.
Elimu ya Uchumi imetolewa na maonyesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiriamali yamefanyika ili kujikwamua kiuchumi.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa