Shirika la Community Development Empowerment Organization (CDEO) laikabidhi Shule ya Sekondari umoja King'ori iliyopo halmashuri ya Wilaya ya Meru kompyuta mpakato 20 na printa moja.
Mkurugenzi wa Shirika hilo la CDEO Ndg. Terevael Nassari amesema shirika hilo katika kushirikiana na seriali na kuchangia maendeleo kwenye sekta ya elimu limetoa komputa 20 kwa shule ya sekondari Umoja king'ori ili kukamilisha darasa la TEHAMA kwani awali liliwezesha Maktaba ya kidijitali kwa kutoa compyuta mpakato moja yenye hadhi ya Maktaba na uwezo wa kuhudumia compyuta nyingine 100 kudurusu masomo mengine mbalimbali wanavyohitaji.
Aidha Nasari amesema CDEO inalenga kushirikiana na jamii, Serikali na wadau wengine katika kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi ambapo ameiomba serikali kuwezesha ufungaji wa umeme shuleni hapo ili kupunguza gharama ya kutumia genereta.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi Waliohudhuria hafla hiyo ya kukabidhi komputa Ndg. Wiliam Urio Amewashukuru na kuwapongeza wadau wa CDEO ambao wajumbe wake wengi ni vijana Wazawa wa king'ori kwa kutoa vifaa hivyo ambapo ametoa wito kwa vijana wengine kuiga mfano huo ili kuhakikisha wanachochea Maendeleo kwenye jamii zao.
Aidha, Mzee Urio ametoa Wito kwa wanafunzi kuweka jitihada kwenye masomo ili kupata elimu bora na kufikia malengo yao kwani Serikali imeshaweka mazingira wezeshi ya kusoma kwa kuwajengea madarasa na kuwawekea samani " *Enzi zetu tulitembea umbali mrefu kwenda shule, madarasa yalikuwa hayana milango, sakafu wala madirisha"* ameeleza Urio.
Mhe. Lukas Kaaya Diwani wa Kata ya King'ori amewashukuru Wadau hao wa CDEO kwa mchango utakao leta manufaa katika suala zima la elimu .
Mhe. Kaaya amesema katika Kata ya King'ori kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi na wadau kushiriki katika masuala ya maendeleo baada Ya Serikali ya awamu ya sita kutoa fedha katika sekta ya elimu, afya, miundombinu ya barabara nk "hakika awamu ya sita imetugusa King'ori, imetupa milioni 500 za ujenzi wa kituo cha afya Mareu ,milioni 40 za ujenzi madarasa mapya mawili na samani katika shule ya sekondari Umoja King'ori, milioni 25 kukamilisha maboma 2, pia tumepewa fedha kukamilisha madarasa 3 katika shule ya Umoja Kingori sekondari, vilevile tumenufaika na ujenzi wa barabara ya Malula King'ori kwa kiwango cha changarawe" Amefafanua Kaaya
Mwakilishi wa Mkurugenzi kwenye hafla hiyo Lusajo Ndimbwa, ambaye pia ni afisa elimu taaluma idara ya sekondari amelipongeza shirika la CDEO kwa kutoa komputa mpakato 20 na printa moja kwa shule ya Sekondari Umoja King'ori na kutoa wito kwa uongozi wa shule kuzitunza sambamba na kuona namna ya kuwajengea uwezo zaidi walimu kwenye suala la TEHAMA.
Mkuu wa Shule ya Sekondari King'ori Mwl. Fred Lubida amelishukuru shirika la CDEO kwa kwa kutoa komputa 20 na Printa moja na kuahidi kuzitunza na kuzitumia kikamilifu ili kuleta tija na kuwezesha shule kusajili somo la TEHAMA.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa