Wakulima wa zao la pareto katika Kijiji Cha Kisimiri juu Wilayani Arumeru wahamasika kulima zaidi zao la pareto ambalo hustawi vyema katika kijiji hicho ikiwa ni zao jipya la biashara lisilo hitaji matumizi ya viuatilifu na hutumia mbolea ya samadi .
Godfrey Motika ambaye ni mkulima wa muda mrefu wa zao la pareto amesema zao hilo limemsaidia kujenga nyumba na kuitunza familia yake(poligamy) kwa kipindi chote .
Naye Orneng Irac ambaye ni mkulima wa pareto na Kiongozi wa mila ameiomba Serekali kutengeneza barabara ya kuingia Kijiji hicho kwani ni changamoto kubwa kwenye kilimo cha pareto ambapo imewalazimu wakulima kutumia gharama kubwa ya Usafiri kupeleka mazao sokoni.
Irac ameliomba Baraza la Pareto Tanzania (PCT) kuongeza idadi ya miche ya pareto inayotolewa kwa wakulima.
Afisa kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Meru Bi. Digna Masawe amesema zao la kilimo cha parato ni zao lisilo na gharama kubwa za uzalishaji kwani mkulima akiwa na Mtaji wa Shilingi laki 5 anaweza kulima ekari moja na kupata zaidi ya milioni nne kwa mchumo wa awamu ndani ya kipindi cha miaka mitatu kwani bei elekezi ya zao hilo ni Tsh.2,600 kwa kilo lakini mkulima anaweza kuuza hadi Tsh.4000 kwa kilo kutoka na ubora .
Masawe amesema Kuna haja ya wakulima wa Kisimiri kulima zaidi zao la pareto ambalo hustawi kwenye mwinuko ambalo ni miongoni kwa mazao ya kimkakati hapa nchin na huchukua muda usiozidi miezi mitatu tuu ili kuanza kuchumwa.
Afisa kutoka PCT Godluck Tairo amesema zao la pareto linamanufaa kwani Serikali katika kuhakikisha mkulima ananufaika imeongeza bei ya pareto kutoka Tsh. 2,100 kwa kilo hadi Tsh.2,600 kwa kilo na PCT itahakikisha inato miche kwa wakulima sambamba na kuendelea kuwalipa kwa wakati .
Mhe.Dauson Urio, diwani wa Kata ya Uwiro ametoa wito kwa wananchi wa Kijiji Cha Kisimiri juu kujikita kwenye kilimo cha zao la Pareto ili kujikwamua kiuchumi "rai yangu kwenu kilimo hichi cha pareto kiitambulishe Kisimiri juu"amehimiza mhe.Urio
Urio amesema Serikali ipo bega kwa bega kuhakikisha changamoto ya barabara inatatuliwa kwani sintofahamu ya ukarabati wa barabara ya kuingia Kijiji hapo imeshatatuliwa na ukarabati umeanza, pia taarifa yake imetolewaa kwa wakala wa barabara mijini na Vijiji TARURA .
Mhe.Dauson Urio diwani wa Kata ya Uwiro.
Wananchi wa Kijiji Cha Kisimiri juu wakati wa utoaji elimu ya kilimo cha zao la pareto.
Wananchi wa Kijiji Cha Kisimiri juu wakati wa utoaji elimu ya kilimo cha zao la pareto.
Wananchi wa Kijiji Cha Kisimiri juu wakati wa utoaji elimu ya kilimo cha zao la pareto.
Orneng Irac ambaye ni Kiongozi wa mila na mkulima wa zao la pareto akizungumza wakati wa utoaji elimu ya kilimo cha zao hilo.
Afisa kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Meru Bi.Digna Masawe akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Kisimiri juu.
Afisa kutoka PCT Godluck Tairo akizungumza na Wananchi wa kijiji Cha Kisimiri juu.
Bi.Neema Munisi ,afisa ushirika akitoa elimu juu ya umuhimu wa vyama vya ushirika.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa