Timu ya Watumishi Halmashauri ya Wilaya ya Meru imeanza kwa kishindo kujinoa vikali kwa ajili ya mashindano ya siku ya Wafanyakazi Duniani ya Mei Mosi.
Timu hiyo inayoshiriki mashindano ya Mei Mosi yatakayofanyika jijini Arusha imeendelea kufanya vizuri baada ya kupata matokeo ya suluhu dhidi ya timu ya Wizara ya Afya Kwenye mchezo uliofanyika katika viwanja vya Agha khan jijini Arusha. Matokeo hayo ni baada ya Timu hiyo kuining'iniza Timu ya Tume ya Mịpāngo hapo jana kwa kupata ushindi mnono wa goli 8 kwa 1 kwenye mchezo wa ufunguzi wa Mashindano hayo yanayoendelea jijini Arusha Halmashauri ya Wilaya ya Meru inawakilishwa na Timu 2 ambazo ni mpira wa Miguu na Mpira wa Pete.
Kauli mbiu ya Mei Mosi 2024: "Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao bora na Kinga dhidi ya Hali ngumu ya Maisha".
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa