Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu J. Makwinya mapema hii Leo amefika katika kituo kilichopo kitongoji cha Nganana kata ya kikwe kituo alichojiandikisha Kwa Lengo la kupiga Kura.
Mara baada ya kupiga Kura msimamizi wa Uchaguzi amethibitisha kufunguliwa Kwa Vituo vyote saa 2 kamili Asubuhi na kusema hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza na watu wanaendelea kupiga Kura Kwa wingi
Aidha ameendelea kuwasisitiza Wananchi kufika kwenye Vituo Kwa muda uliowekwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Anwani: P.o. Box 462 Usa River
Simu ya Mezani: (+ 255) 272970482
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@merudc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Wilaya ya Meru. Haki zote zimehifadhiwa